SIASA
Ndugai ataka viongozi wa CCM Zanzibar kuandaa mazingira ya ushindi mwaka 2020
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa, Ndugu Job Ndugai
amewataka Wanachama na Viongozi wa CCM Visiwani Zanzibar kuendeleza
harakati za kuandaa mazingira rafiki ya kukipatia ushindi Chama mwaka
2020.
Rai hiyo ameitoa mara baada ya kuwasili leo Zanzibar kwa ajili ya ziara
ya kutembelea Mikoa miwili ya kichama ambayo ni Mkoa wa Kaskazini Unguja
na Mkoa wa Kusini Unguja.
Ndugai ambaye ni Mlezi wa Mikoa hiyo,amesema kila mwanachama anatakiwa
kujipanga kuhakikisha CCM inaendelea kubaki madarakani kwa ridhaa ya
wananchi.
Katika maelezo yake Ndugai, amewashukru viongozi na wanachama wa CCM wa
Mikoa hiyo kwa mapokezi makubwa jambo aliloeleza kuwa hali hiyo
imemuongezea ari,hamasa na ujasiri wa kufanya ziara yake ufanisi mkubwa.
Amewasisitiza wanachama wa Mikoa hiyo kuendeleza sifa na heshima ya
maeneo yao yanayosifika kwa kuwa ngome imara za Chama Cha Mapinduzi.
Aidha Ndugai ameeleza kuwa CCM inaendelea kuimarika Kisiasa, Kiuchumi,
Kidemokrasia na kimfumo huku baadhi ya vyama vya siasa vikiendelea
kudhoofika kisera na kisiasa.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,
amemwakikishia Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia ni Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa hali ya kisiasa katika
Mikoa anayoilea ipo shwari kutokana na historia nzuri ya maeneo hayo
ambayo ndio yenye azna kubwa ya mtaji wa kisiasa wa CCM.
Amesema kuwa jukumu la ulezi wa Mikoa ni kubwa hivyo anaamini kuwa
Mhe.Job Ndugai atafanya atafanya ziara yake hiyo ya kujitambulisha kwa
wanachama pamoja na kuwapatia nasaha mbali mbali za kuwaongezea hamasa
ya kuendelea kuwa wazalendo wa CCM na Taifa kwa ujumla.
Ziara hiyo ya Ndugai ni ya siku tatu atatembelea maeneo mbali mbali na
kuzungumza na wanachama kupitia vikao vya ndani sambamba na kukagua
miradi iliyotekelezwa kupitia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya
mwaka 2015/2020.
Breaking News: Mbunge wa TEMEKE Abdallah Mtolea Ajivua Uanachama wa CUF Akiwa Ndani ya Bunge Leo
Mbunge
wa Temeke, Abdallah Mtolea (CUF), ametangaza kujivua unachama wa chama
chake na kujiuzulu ubunge, akitaja sababu kuwa ni mgogoro kati ya
wanachama wanaomtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti wa chama
hicho na wale wanaomtambua Maalimu Seif Shariffu Hamad, kuwa Katibu
Mkuu.
Tofauti na wabunge wengine, Mtolea alitangaza uamuzi wake ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wabunge wakijadili Muswada wa Sheria Ndogo ya Fedha wa mwaka 2018.
“Sijui mnaoshangilia mnashangilia nini, lakini tulio ndani ndiyo tunaujua huu mgogoro, imefikia hadi hatua ya kutishiana maisha huko mitaani,” amesema Mtolea.
“Kwa hiyo nawashukuru wote kuanzia wewe Spika (Job Ndugai) kwa ushirikiano tuliokuwa nao hapa, Waziri Mkuu, wabunge wenzangu haswa wa kambi ya upinzani ambao mmekuwa karibu na mimi hata wale ambao hawatafurahishwa na uamuzi wangu huu.
“Najiuzulu nikiwa bado natamani kuwahudumia wananchi wa Temeke kwa hiyo nawakaribisha vyama vyote kuanzia Chadema, NCCR na CCM kujadiliana namna tutakavyoweza kushirikiana,” amesema.
Mtolea pia alitoa shukrani kwa wanachama wote wa CUF ambao hawamuungi mkono Profesa Lipumba.
Baada ya kutoa kauli hiyo, Spika alimtaka kutoka nje ya ukumbi wa Bunge ambapo Mtolea alitii amri hiyo na kumpa mkono Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira Kazi na Vijana, Jenister Mhagama, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini huku Mbunge wa Tunduma (Chadema), Pascal Haonga akikataa kupewa mkono.

Hakuna maoni