UREMBO
Njia ya Asili ya Kuondoa Mafuta Katika Ngozi Ya Uso Wako
ngozi yenye mafuta huwa kerosana kwa wakina dada hasa usoni kwa
sababu moja ya adhabu ya ngozi yenye mafuta ni kuwa na chunuzi nyingi
sana usoni. watu wengi wanaangaika na tatizo hilo na hata kuanza kutumia
vipodozi vikali wakati kuna njia rahisi ya asili inaweza kusaidia
kuondoa tatizo hilo.
mahitaji
- ute mweupe wa yai
- vijiko vitatu vya juisi ya limao
NB:Mchanganyiko huu ulainisha ngozi ya uso na kuwa laini lakini pia upunguza ukubwa wa matundu ya ngozi ya uso wako.
JINSI YA KUWA NA NGOZI YA USO YENYE MVUTO KWA NJIA YA ASILI
Usafi wa uso ni
moja ya mambo muhimu sana kwa mwanamke au mwanaume yeyote yule ambaye
anapenda kuwa nadhifu na mwenye mvuto. Kumbuka “reception ndio kila kitu “.
Unapokutana na mtu sura yako na mwonekano wa sura yako ndio kitu cha kwanza
kinachomtambulisha kwamba wewe ni nani na upo kwenye hali gani.
Kuna njia nyingi za
kuufanya uso wako uvutie na kupendeza. Leo tutaongelea zaidi jinsi ya kusafisha
uso kwa njia ya asili. Mie hupenda
kutumia njia ya asili sababu ni rahisi kupata vifaa na ni nafuu . Pia mtu
anaweza kufanya kwa mazingira yoyote yale. Na matumizi ya vitu vya asili kwenye
mwili husaidia kupunguza sumu mwilini kwani kitumia vipodozi vyenye kemikali
husababisha miili yetu kujaaa sumu.
Njia ya asili ya
kusafisha na kupendezesha mwili ninayokueleza leo inahitaji vitu vikuu vinne :
asali, sukari, maziwa, na limao.
Haijalishi aina gani ya
ngozi unayo , njia hii ya asili inaweza kutumika kwa aina yoyote ile ya ngozi
iwe ngozi yenye mafuta au ngozi kavu.
Kiasi cha mahitaji
yanayohitajika:
- Kijiko kimoja cha asali
- Kijiko kimoja cha sukari
- Kijiko kimoja cha maziwa
- Kijiko kimoja cha limao
Utaratibu wa kusafisha
uso
Weka mahitaji hapo juu kwenye chombo kilicho kisafi,
changanya vitu vyako mpaka vilainike, viache kwa muda wa dk 10 ili viweze
kuchanganyikana vizuri na na sukari iweze kuyayuka vizuri.
Baada ya mchanganyiko
wako kuwa tayari chukua kipande cha pamba kilicho kisafi tumia kupakia
mchanganyiko wako usoni . Na kumbuka ni vizuri uso ukiwa mchafu na upaswi
kuosha uso alafu ufanye zoezi hili.Baada ya kupaka mchanganyiko wako
usoni kaa kwa dk 15 .
Baada ya hapo chukua
maji ya uvuguvugu, kitaulo kisafi na sabuni ya kipande “vizuri kutumia sabuni
ya kipande maana haina kemikali nyingi” tumia kitambaa kuoshea uso wako
pamoja na sabuni.
Basi baada ya hapo
umekuwa umemaliza zoezi lako la usafi wa ngozi yako
Kumbuka njia hii aina madhala yoyote na haibadilishi rangi au muonekano wa ngozi yako na unashauliwa kufanya mara kwa mara ili kukupa mvuto zaidi.
EPUKA NYWELE ZINAZOKATIKA KWA KUTUMIA KITUNGUU MAJI
Kitunguu
maji kina sulphur ambayo husaidia kutengeneza tishu za collagen katika
mwili ambapo collagen husaidia kunurisha nywele na ngozi. Hivyo
tunaweza kusema kuwa kitunguu maji husaidia kukuza nywele na kwa wale
wenye nywele za kukatika, kupaka kitunguu maji mara kwa mara kinaweza
kusaidia kupambana na tatizo hilo.
Je utatumiaje kitunguu ili ufaidike na kitunguu maji kwa nywele zako. Soma zaidi hapa chini.
Jinsi ya kuandaa
- Chukua kitunguu kimoja au viwili kutegemeana na ukubwa wa kitunguu chenyewe. Fuata hatua zifuatazo:
- Osha vizuri kitunguu au vitunguu na kisha ukimenye au uvimenye
- Kata kitunguu au vitunguu vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga au kutwanga
- Saga kwenye brenda au twanga kwenye kinu , njia yoyote ile ambayo kwako ni rahisi kwako. Visage au vitwange mpaka vilainike kabisa ili uweze kutoa maji kwa urahisi.
- Ukishasaga au kutangwa vitunguu , vichuje vizuri ili upate maji maji .Zingatia usiweke maji kwa hivi vitunguu.
Jinsi ya kupaka
Nywele sio lazima ziwe safi maana unapaswa kuziosha baada ya kupaka maji ya vitunguu.
- Chukua pamba ambayo utatumia kupaka hayo maji ya vitunguu kwenye nywele zako. Paka zile sehemu ambazo nywele zimekatika. Unaweza pia paka kichwa kizima.
- Baada ya kupaka unapaswa kuvaa kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ili kuweza kupata joto . Tahadhali usikae kwenye mashine ya steam au dryer.
- Ukiwa na kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ya nywele zako , ukae hivyo hivyo kwa masaa manne hadi matano.
- Baada ya hapo unaweza kuosha na kukausha nywele zako na kuweka style yoyote ile.
Hitimisho
Ni
vema kufanya zoezi hili la kupaka vitunguu walau mara mbili kwa mwezi.
Ikiwa harufu ya kitunguu ni kali, unaweza weka asali kidogo kwenye maji
ya vitunguu.
Kwa matokeo mazuri ya kukuza na kutunza nywele zako tumia vitunguu vidogo kufanya zoezi nililoeleza hapo juu.
Njia Sahihi Ya Asili Ya Kukuza Nywele Zako
1.Zifahamu aina ya nywele zako
kitu cha kwanza kujua ni kizifahamu nywele zako, kuna watu wanakaa na nywele bila kujua nwele zake ni za iana gani,Jinsi ya kujua aina ya nywele zako , chomoa nywele moja katika kichwa chako na uhakikishe imetoka na kale kamzizi kanakokuwa na rangi ya weupe ivi, kisha dumbukiza unywele huo kwenye glasi yenye maji na angalia kama unywele uo unaleta matokeo gani,kama itazama mara moja na haitanyanyuka tena basi jua nywele yako inanyonya unyevu kwa haraka ivyo inaitaji kuwa na unyevu unyevu na kama .
Loading...
kama ilivyo kiu kwa binadamu, ndivyo hivyo nywele huitaji maji, kwaio kipindi unapokuwa unaosha nywele zako kabla ya kuzipaka mafuta ya kulinda nywele zako jitahidi kuwa una fanya deep condition ili kuzifanya zibaki na unyevu .
3.Usafi wa ngozi na nywele zenyewe pia.
Kuna watu wanasema kuwa nywele zikioshwa mara kwa mara zinadumaa, lakini ulishawahi kujiuza endapo wewe utakaa bila kuoga.Nywele zinahitajika kuwa safi na ngozi yake pia ili kuifanya ngozi kufunguka na sio kufungwana ule uchafu wa mafuta.Matundu yanapokuwa wazi ndio ufanya nywele kuweza kujitokeza ivyo jitahidi kuosha nwele na kuhakikisha kuwa ngozi yako ni safi.
4. Chagua Mafuta bora ya kupaka
Jitahidi kuchagua mafuta mazuri kwa ajili ya nywele zako.sio kila mafuta yanafaa kupaka katika nywele zako ingawa mafuta ya nazi ni mazuri zaidi au mafuta ya olive.kitu kizuri ni kuzijua nywele zako kwanza ndipo utaweza kujua pia bidhaa bora ya mafuta kwa ajili ya nywele.Ukishindwa ni bora kuonana na wataalamu wa mambo ya urembo.
5.Epuka kuzisumbua nywele kila wakati.
Ni vizuri kuwa unachana nywele kwa muoekano mzuri wa sura yako na nwele pia, lakini kitendo icho ufanya nywele kuwa zinapuputika sana,jitahidi kuwa unazisuka ili kuzifanya zikue pia.Kuchana chana nywel ni kuzisumbua.
Inawezekana inakuwa ni ngumu kutambua nywele zake zinahitaji mafuta ya aina gani, au bidhaa gani ni bora zaidi kwa nywele zako, ni vizuri pia kuonana na wataalamu ili kuzisaidia nywele zako.
JINSI YA KUKUZA NYWELE KWA KASI, NDANI YA MWEZI MMOJA
Na
wakati unapaka mafuta kichwani kichwa kiinamishe chini, kiangalie chini
ndio upake mafuta kichwa chako husaidia msukumo wa damu kufikia katika
kichwa vizuri na kupata stimulation kwa kutumia ncha za vidole huku
ukifanya massage kichwa taratibu kwa mda wa dakika tano, ukimaliza anza
kuzichana taratibuu mpaka zilainike na uzibane..
NB:
Jaribu kwa siku uchane nywele mara mbili asbuh na jion, na nywele muda
wote ziwe zenye mafuta. jizoeshe kufanyia massage kichwa chako kila
wakati unaopaka mafuta kichwani. Uhai wa nywele ni mafuta kama ilivyo uhai wa binadamu utakuepo iwapo kuna maji.
Namna bora ya kutunza kucha na kuepuka maradhi shambulizi ya kucha.
Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa
msichana. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni
na sehemu mbalimbali katika maisha kuanzia kutandika kitanda, kupika,
kufanya usafi, kuandika, kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi.
Mikono isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika, kupoteza mvuto wake wa asili na kuharibu afya ya kucha. Hitaji la urembo wakati mwingine humsukuma msichana katika matumizi ya vipodozi vya kupaka kwenye kucha zake ili kukamilisha urembo wake.
Urembo wa vidole na kucha sio lazima ufanyike katika saluni au kwa wataalamu wa kupamba kucha, msichana anaweza kushughulikia afya na urembo wa vidole na kucha zake kwa gharama nafuu na kwa muda ambao mwenyewe anaona unafaa kufanya hivyo hata akiwa nyumbani.
Hii pia itamsaidia Msichana kuchagua vipodozi salama kwa afya ya kucha zake na mwili kwa ujumla. Ni jambo la muhimu kufahamu kuwa baadhi ya vipodozi vinavyotumika katika urembo wa kucha, vina rangi na sumu zisizofaa kwa afya. Sumu kama vile ‘Formaldehyde na Toluene’ zinazopatikana katika baadhi ya rangi za kucha zina madhara kwa afya ya msichana.

Ni kweli kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha ya msichana
lakini pia ni busara kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na
uzuri. Afya ya mwili na kucha za msichana kwa ujumla hutegemea chakula
bora chenye protein, madini na vitamini na siyo rangi na vipodozi.
Upungufu wa vitamini A, B Complex, proteni, madini ya chuma na chokaa (kalishiamu) mwilini husababisha kucha zipoteze afya yake ya asili. Kucha ambazo hazina afya zinaweza kuoza, kukauka, kupinda, kupasuka au kuwa na umbo kama kijiko. Magonjwa ya kuvu (fungus), na baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusi pia huharibu afya ya kucha. Mojawapo ya athari za dawa za kupunguza makali ya VVU aina ya Zidovudine (ZDV) ni kucha kuwa na rangi nyeusi.
Kwa ajili ya afya bora ya kucha msichana anashauriwa kula mboga za majani, maharage, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha. Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.

Kucha za msichana zinatakiwa zisiwe ndefu ili kuepuka utunzaji wa vimelea vinavyosababisha magonjwa na kurahisisha utunzaji na usafi wa kucha. Kucha ndefu zinaweza kuwa chanzo cha hatari kwa afya ya msichana na familia yake hasa pale msichana anapohusika na uandaaji wa chakula cha familia. Katika familia nyingi, hasa familia za kiafrika wasichana ndio wanaobeba wajibu na majukumu ya kuandaa chakula cha familia.
Kwa afya nzuri ya kucha, msichana anashauriwa kukata kucha zake ili ziwe fupi kadri anavyotaka kwa kutumia ‘nail cutter’ au mkasi mdogo au wembe mpya ambao haujatumiwa na mtu mwingine. Kuchangia nyembe za kukatia kucha si salama kwani kunaweza kuwa njia mojawapo ya kusambaza vimelea vya magonjwa hatari ya kuambukiza kama vile virusi vinavyosababisha UKIMWI na ugonjwa wa homa ya ini.
Ni vizuri kulainisha ncha za kucha baada ya kuzikata kwa kutumia tupa ya kucha (nail file) na kuzisugua kuelekea upande mmoja ili kuepuka kucha
zisivunjike au zisisababishe michubuko ya ngozi wakati wa kujikuna.
Kusugua kucha kwa kwenda mbele na nyuma kunaweza kusababisha kucha
zivunjike kwa urahisi na haraka.
Kwa afya njema ya kucha, msichana pia anashauriwa asifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni.
Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus)

Hakuna maoni