MICHEZO
Meneja Man U awaomba radhi mashabiki
Ole Gunnar Solskjaer, ambaye ni
meneja wa klabu ya Manchester United amewaomba radhi mashabiki wa timu
hiyo baada ya kuchezea kichapo cha 4 bila toka timu ya Everton katika
mchezo wa ligi kuu ya England.
” Nataka niombe radhi kwa mashabiki wote wa klabu hii tulizidiwa
katika kila idara ila tulipata hamasa ya kutosha toka kwa mashabiki wetu
na tutajitahidi kufanya vyema siku ya jumatano.” amesema Ole Gunnar
Solskjaer.Ole Gunnar Solskjaer amezungumza hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
-
Mchezaji mkongwe aponda uamuzi wa Man United kuhusu Solskjaer
United wamepoteza jumla ya michezo 6 ya hivi karibuni ikiwa ni michezo nane katika michuano yote waliyokuwa wakishiriki ikiwemo ligi ya mabingwa barani ulaya.
Mchezo dhidi ya Everton ulikuwa ni muhimu sana kwa klabu hiyo katika mbio za kuwania nafasi nne za juu ili kuweza kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao.
Manchester United watashuka dimbani tena siku ya Jumatano kuwakabili majirani zao Manchester City wanaouwania ubingwa kwa mara ya pili mfulizo.
Hiki Hapa Kikosi Cha Simba Dhidi Ya Tp Mazembe
Tetesi za Soka Ulaya 26.03.19: Pogba, Mbappe, Mane, Neymar, Felix, Umtiti
Kiungo Mfaransa Paul Pogba, 26,
amefikia maamuzi ya kuihama Manchester United mwishoni mwa msimu na
anafikiria kwenda Ligi ya Uhispania ama Italia. (AS - in Spanish)
Mshambuliaji wa Liverpool na Senegali Sadio Mane, 26, pia anatakiwa na Real Madrid mwishoni mwa msimu. (Marca - in Spanish)Mshambuliaji wa Brazil Neymar yumo katika mazungumzo ya kuongeza mkataba na klabu yake ya Paris St-Germain, kwa mujibu wa baba wa mchezaji huyo. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 amekuwa akihusishwa na mipango ya kuhamia Real Madrid. (ESPN)
Benfica wanataka kuongeza kipengele kigumu kwenye mkataba wa mshambuliaji Mreno Joao Felix ili kuzipunguza makali klabu ambazo zinzmnyemelea mshambuliaji kinda huyo. Manchester United na Juventus zimekuwa zikihusishwa na kumtaka Felix, 19. (Tuttosport - in Italian)
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ameazimia kumsajili Mshambuliaji kinda wa Ufaransa na klabu ya Paris St-Germain Kylian Mbappe, 20, kwa udi na uvumba, na yupo tayari kutangaza dau nono la pauni milioni 240. (France Football - in French)
Barcelona wanaweza wakawauzia Manchester United mlinzi wao wa kati Samuel Umtiti mwishoni mwa msimu, japo beki huyo mwenye miaka 25 anataka kusalia Camp Nou. (Mail)
Beki wa Chelsea Christensen amesema kuwa wachezaji wa klabu hiyo wametaarifiwa kuwa hawataruhusiwa kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu endapo marufuku ya usajili inayoikabili klabu hiyo haitaondoshwa. (Times)Kiungo wa Manchester United raia wa Serbia Nemanja Matic amesema nataka kocha wa mpito wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer pamoja na benchi lake lote la ufundi wapewe kazi ya kudumu katika klabu hiyo. (ESPN)
Kiungo wa Manchester United raia wa Uhispania Ander Hererra, 29, amesema ni jambo la kawaida kuhusishwa na kutaka kuhamia klabu ya Paris St-Germain kutokana na kusalia miezi mitatu tu mpaka mkataba wake na Old Trafford kufikia tamati. (El Periodico - in Spanish)
Arsenal pia wanataka kumsaini Hererra kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu. (Mail)
Kombe la Carabao: Wasiwasi kuhusu Kevin de Bruyne licha ya ushindi wa Man City dhidi ya Fulham. Manchester City walifanikiwa kuwalaza Fulham 2-0 kwenye mechi ya Kombe la Ligi iliyochezwa Alhamisi lakini wameingiwa na wasiwasi kuhusu kiungo wao nyota Kevin de Bruyne.
De Bruyne alichechemea na kuondoka uwanjani baada ya kuonekana kuumia dakika tatu kabla ya mechi kumalizika.
Nyota wa mechi hiyo alikuwa kinda Mhispania Brahim Diaz ambaye alifunga bao moja kila kipindi, dakika ya 18 na 65, hayo yakiwa mabao yake ya kwanza kufungia timu kubwa ya Manchester City.City sasa watakutana na mshindi wa mechi kati ya Leicester na Southampton kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambayo hufahamika kama Kombe la Carabao.
Mbelgiji De Bruyne mwenye miaka 27 alikuwa ameanza mechi kwa mara yake ya pili pekee msimu huu tangu alipopata jeraha kwenye kano za goti lake la kulia mwezi Agosti.
"Anachunguzwa na madaktari," alisema meneja wa City Pep Guardiola baada ya mechi.
"Hatujafahamu kufikia sasa iwapo hakuna kitu chochote kibaya kimemtendekea au kama ni kitu kibaya."
De Bruyne alikuwa amecheza vyema sana na kuonekana kujituma uwanjani lakini aliondoka uwanjani akiwa anagusa goti lake la kushoto, na moja kwa moja akaelekea chumbani kupokea matibabu.
Viongozi hao wa Ligi ya Premia kwa sasa walikuwa wamefanya mabadiliko 10 kwenye kikosi chao kilicholaza Tottenham Jumatatu lakini bado waliwazidi nguvu Fulham waliotumia kikosi chao cha kwanza, walikuwa na makombora 27 yaliyolenga goli wakilinganishwa na wageni wao waliolenga goli mara tano pekee.
Alikuwa amecheza dakika 150 pekee kwa jumla msimu wa 2018-19 kabla ya mechi hiyo na hakuonekana kuwa na uchovu.
Alishambulia mara kwa mara na alionekana kujizatiti kuupata mpira tena kila City walipopokonywa.
Alikabili wapinzani na kushinda mpira mara saba, na akazuia mpira mara tatu.
"Ni kawaida kwa watu kusema mchezaji ameonyesha kiwango cha kuwa stadi zaidi duniani, lakini hautakuwa unaongeza chumvi ukisema kuhusu uchezaji wa De Bruyne," Pat Nevin aliyekuwa akichambua mpira katika BBC Radio 5 alisema.
Huku kukiwa na mechi nyingine tano za kuchezwa Novemba, ambapo miongoni mwake kuna mechi ya debi dhidi ya Manchester United uwanjani Etihad, Guardiola atatumai kwamba De Bruyne hakuumia sana.
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 02.11.2018: Ramsey, Fabregas, Suarez, Gomez, Fabinho
Chelsea huenda ikabadili msimamo
kuhusu mpango wake wa kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey,
27,kutokana na kuimarika kwa mchezo wa Ross Barkley, 24, na Ruben
Loftus-Cheek, 22. (Star)
Huku hayo yakijiri, Liverpool imefutilia
mbali uwezekano wa kiungo huyo wa kimaatifa wa Wales ambaye yuko tayari
kuondoka Gunners bila malipo msimu wa joto kujiunga nayo. (Sky Sports)Kiungo wa kati wa Mhispania Cesc Fabregas, 31, atalazimika kusubiri hadi mwaka mpya kabla ya kuanza mazungumzo ya kandarasi mpya na Cheasea . (Evening Standard)
Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 31, anasema Barcelona hivi karibuni itaanza kumtafuta mtu atakaechukua nafasi yake licha ya kufunga hat-trick katika mechi ya El Clasico. (Sport 890, via Sun)
Liverpool inajiandaa kumpatia kandarasi mpya mlinzi wa England defender Joe Gomez, 21, miaka tatu na nusu hata kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Brazil Fabinho huenda akaondoka Liverpool miezi sita tu baada ya kuhamia Anfield kwasababu ''ameboeka''. (Le Parisien - in French)
Meneja wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amesema "Hatutapoteza muda wetu kujadili hilo" alipoulizwa kuhusu tetesi za Real Madrid kutaka kumpatia kazi kama meneja wake mpya. (AS, via VTM Nieuws)
Mazoezi ya kiungo Azam ni baiskeli tu!
nadaiwa tatizo la kiungo wa Azam FC, Frank Domayo alilipata kwenye timu
ya Taifa Stars ilipokuwa ikijiandaa na mechi dhidi ya Cape Verde ambazo
zilikuwa mbili mfululizo za kuwania nafasi ya kufuzu Fainali za Mataifa
ya Afrika (AFCON).
Hakuna maoni