HABARI
Rais Magufuli Awatangazia Kiama Majangili
Rais Magufuli amewatangazia kiama wauaji wa tembo ndani na nje ya nchi na kumtaka Mkuu wa Hifadhi ya Selous kujipanga vizuri.
Rais Magufuli aliyasema hayo jana, wakati akizindua barabara ya kilomita 193 ya Namtumbo, Kilimasera, Matemanga hadi Tunduru, katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
“Washtakiwa wa eneo hili wengi ni wanaoua tembo, unakuta Watanzania wanashirikiana na majangili wa nchi jirani, wakiua tembo huku wanawapeleka kule na wakiua tembo kule wanawaleta huku.
“Mtandao wote tumeshaujua, mkae mwendo wa mchakamchaka, wapo wengine wanashirikiana na viongozi, ninafahamu circle.
“Tunataka Selous iwepo, sasa anayehusika na Hifadhi ya Selous ajipange vizuri, wengine wanaoshirikiana na kutengeneza mtandao ni watendaji kazi wa Selous,” alisema.
Akizungumzia barabara hiyo, Rais Magufuli alisema ujenzi wa kilomita 193 si kazi ndogo na umetumia zaidi ya Sh bilioni 173.3.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yatangaza Kuanza Uboreshaji Daftari la Wapiga Kura
Na Margareth Chambiri
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kufanya zoezi la uandikishaji wa
Wapiga Kura kwa majaribio katika Kata mbili za Kibuta iliyopo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani na Kihonda katika
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mkoani Morogoro.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage Jijini Dar es Salaam leo (Jumanne Tarehe 26. 03. 2019) imesema Uandikishaji huo wa Majaribio utakaoanza Machi 29, hadi Aprili 04, 2019 utafanyika katika vituo 20 vya kuandikisha Wapiga Kura ikiwa ni vituo 10 katika kila Kata.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa uandikishaji huo unalenga katika kuvifanyia majaribio vifaa na mfumo wa Uandikishaji Wapiga Kura ili kubaini changamoto kabla ya kuanza rasmi kwa zoezi hilo.
Imezitaja sifa za watu watakaoandikishwa katika uandikishaji huo kuwa ni raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 au atakayetimiza umri wa miaka 18 siku ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Aidha uandikishaji huo hautawahusu raia walio chini ya kiapo cha utii wa nchi nyingine, aliyebainika kuwa hana akili timamu au yuko kizuizini kama mhalifu mwenye ugonjwa wa akili au yuko kizuizini kwa ridhaa ya Rais.
Taarifa hiyo imeendelea kutaja watu ambao hawatahusika katika majaribio hayo ya uboreshaji kuwa ni mtu aliyehukumiwa adhabu ya kifo na mahakama au anatumikia kifungo kinachozidi miezi sita pamoja na mtu aliyepoteza sifa za kuandikishwa kuwa Mpiga Kura chini ya Sheria za Uchaguzi au Sheria nyingine yoyote inayohusu makosa ya uchaguzi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia inawajulisha wakazi wa Kata hizo zinazofanya Uandikishaji wa Majaribio na ambao walijiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015 kuwa wanaweza kutumia fursa hiyo kuhakiki taarifa zao katika vituo walivyojiandikishia.
Wakati huo huo Tume inatoa fursa kwa Vyama vya Siasa kuweka Wakala mmoja katika kila kituo cha Kuandikishia Wapiga Kura kwa lengo la kushuhudia na kujiridhisha juu ya taratibu zitakazotumika pamoja na changamoto zitakazojitokeza ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kabla ya zoezi rasmi la Uandikishaji.
Tume imevitaka Vyama vyenye nia ya kuweka Mawakala katika uandikishaji huu wa Majaribio kuwasilisha orodha ya majina ya Mawakala na vituo walivyopangiwa kwa Maafisa Waandikishaji wa Halmashauri za Kisarawe na Manispaa ya Morogoro.
Kadhalika Vyama vimetakiwa kuwasilisha nakala mbili za barua za utambulisho zikiwa na picha mbili na nakala mojawapo kati ya Kitambulisho cha Taifa au Kadi ya Mpiga Kura, Pasi ya Kusafiria au Leseni ya Udereva na kwamba kila Chama kitagharamia Wakala wake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo wakati wa uandikishaji huo wa majaribio Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatumia runinga, redio, mitandao ya kijamii na magari ya matangazo kwa ajili ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika zoezi hilo.
Mwenyekiti wa Tume Mheshimiwa Kaijage kupitia taarifa hiyo amewaomba wakazi wa Kata za Kibuta na Kihonda kujitokeza kwa wingi katika Uandikishaji huo wa majaribio na kutoa ushirikiano kwa Tume wakati wote wa utekelezaji wa jukumu hilo muhimu kwa mustakabali wa demokrasia ya Taifa.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi hufanya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mujibu wa Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoipa Tume mamlaka ya kusimamia na kuratibu uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano pamoja na Madiwani kwa Tanzania Bara.
Tume kwa mujibu wa Kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Kifungu cha 21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 inapaswa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili kati ya Uchaguzi Mkuu mmoja na unaofuata.
Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)......Amteua Julius Ndyamukama Kujaza Nafasi Hiyo
Rais
Magufuli amemteua Julius Ndyamukama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuchukua nafasi ya Richard Mayongela
ambae uteuzi wake umetenguliwa na anatakiwa kuripoti Wizara ya Ujenzi
kupangiwa kazi nyingine.
Msajili wa Vyama vya Siasa Atishia Kukifuta chama cha ACT- Wazalendo
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, ametishia kukifutia usajili Chama cha ACT-Wazalendo, kutokana na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa ikiwamo kuchoma moto bendera ya Chama cha Wananchi (CUF).
Mtungi
kupitia barua yake kwa ACT Wazalendo, ametoa siku 14 kwa chama hicho
kuwasilisha maelezo ya maandishi kuwa ni kwanini usajili wake wa kudumu
usifutwe kutokana na kukosa sifa kukiuka Sheria za Vyama vya Siasa na
kutowasilisha ripoti ya ukaguzi kuanzia mwaka 2013-17.
Taarifa
iliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa jana Jumatatu Machi 25,
imesema kutowasilisha ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha 2013/14, chama
hicho kinakuwa bado hakijakidhi matakwa ya Msajili wa Vyama vya Siasa
na hivyo chama hicho pia kinakuwa kimekiuka Sheria ya Vyama vya Siasa
Sura ya 258.
“Aidha,
baada ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi wa kesi Na. 23 ya mwaka 2016,
iliyokuwa inahojiuhalali wa Profesa Ibrahimu Lipumba, Machi 18, 2019,
kumekuwa na matukio ya uvunjifu wa sheria ikiwemo kuchoma moto bendera
za CUF, uliofanya na watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa aliyekuwa
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, wanadai sasa ni wanachama wa ACT.
Kitendo cha kuchoma bendera ya chama cha siasa ni kukiuka kifungu cha
11C, cha sheria ya vyama vya siasa.
“Vile
vile katika mitandao ya kijamii imeonekana video watu wakipandisha
bendera ya ACT kwa kutumia tamko takatifu la dini ya kiislamu (Takbir),
kitendo hiki pia ni kukiuka kifungu cha (9) (1) (c) cha Sheria ya Vyama
vya Siasa inayokataza kuwa na ubaguzi wa kidini kwa wanachama wake na
kifungu cha (9) (2) (a), kinachokataza katiba, sera au vitendo vya chama
cha siasa kuhamasisha au kueneza dini fulani,” imesema taarifa hiyo ya
msajili.
Pamoja
na mambo mengine, msajili amekumbushia onyo lake la Machi 18 mwaka huu
akikemea kitendo cha wananchi wa chama hicho huku akionyesha mshangao
kwa chama hicho kutochukua hatua ya kukemea suala hilo akisema chama
hicho kimeafiki au kilitoa maelekezo kufanyika kwa vitendo hivyo.
“Kutokana
na maelezo hayo, vitendo hivyo vinaakisi ukiukwaji wa dhahiri wa Sheria
ya Vyama vya Siasa ambao pia unasababisha chama chenu kupoteza sifa za
usajili wa kudumu.
“Hivyo,
Msajili wa Vyama vya Siasa anatumia fursa hii kukufahamisha wewe na
wanachama wa ACT-Wazalendo nia yake ya kufuta usajili wa kudumu wa chama
chenu kwa sababu hizo zilizotajwa,” amesema Msajili katika taarifa
yake.
Rais Magufuli Apewa Tuzo ya heshima ya ukuzaji kiswahili Afrika
Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili wa Vyuo Vikuu vya Tanzania (CHAWAKITA)
kimetoa Tuzo ya Heshima kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Magufuli kutokana na mchango wake mkubwa wa kuthamini na
kukuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.
Image result for rais magufuli tuzo
Rais Magufuli
Tuzo hiyo, imetolewa na chama hicho na kupokewa na Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza kwa niaba ya
Rais Magufuli.
Alipokea tuzo hiyo juzi mjini Morogoro wakati akifunga kongamano la 11
la kitaifa la Chawakita lililofanyika Chuo Kikuu cha Waislamu cha
Morogoro.
Kongamano hilo la siku nne lilibeba kaulimbiu inayosema, “Kiswahili,
Hazina ya Afrika kwa Maendeleo Endelevu” na kuandaliwa kwa tuzo kwa
washindi wa uandishi wa vitabu vya hadithi fupi pamoja na ya heshima
ambayo aliyotunukiwa Rais Magufuli kutokana na anavyoenzi na kukitilia
maanani Kiswahili.
Pia tuzo nyingine ya heshima ilitolewa kwa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo kutokana na mchango mkubwa wa wizara hiyo katika
kusimamia na kuendeleza lugha ya Kiswahili nchini.
Waziri Lugola Asema Mkoa Wa Dar Es Salaam Unaongoza Kwa Biashara Haramu Ya Binadamu Nchini.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Mkoa wa Dar es
Salaam unaongoza nchini kwa kufanya biashara haramu ya kusafirisha
binadamu huku akitoa onyo kali kwa wanaojihusisha na biashara hiyo.
Akizungumza kabla ya kufungua mafunzo ya siku tano ya Watekelezaji wa sheria ya kuzuia biashara hiyo haramu, katika hoteli ya Ngalawa, mjini Unguja, Zanzibar, Lugola amesema wanaofanya kazi hiyo waiache mara moja maana Serikali itawashughulikia.
“Tatizo hili, linaweza onekana likawa dogo, lakini ukweli ni kwamba sote tunafahamu ni kubwa na limeendelea kukua kila mwaka. Uzoefu wa kiutendaji kutoka Sekretareti hususani kutokana na wahanga wanaookolewa unaonyesha kwamba biashara hii inafanyika sana Mkoa wa Dar es Salaam Tanga, Mwanza, Kigoma, Geita, Dodoma, Singida, Arusha, Manyara, Shinyanga na Tanzania Zanzibar,” alisema Lugola.
Lugola alisema licha ya changamoto hizo, lakini Serikali katika kipindi cha kuanzia Januari mpaka Disemba 2018 imefanikiwa kuwaokoa jumla ya Watanzania 147 waliokuwa wahanga wa biashara haramu ya usafirishaji binadamu. Kati ya wahanga 141walikuwa wakitumikishwa katika mikoa mbalimbali nchini.
Pia Lugola alisema wahanga 6 walikuwa wakitumikishwa nje ya nchi ambapo watano walikuokolewa kutoka Thailand na mhanga mmoja kutoka Malasia, na Mhanga mmoja aliokolewa hapa nchini alipokuwa akitumikishwa na taratibu za kumrudisha kwao Msumbiji bado zinafanyika.
“Napenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa hatutamuacha salama mtu yeyote, wanaojihusisha na biashara hii waiache mara moja kabla mkono wa sheria haujawafikia,” alisema Lugola.
Aidha, Lugola alisema Serikali ya Tanzania, haijaikataza Watanzania kufanya kazi nje ya nchi, bali imeweka taratibu zenye lengo za kumlinda Mtanzania na madhara yatokanayo na biashara hiyo haramu.
Kwa upande wake, Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara hiyo Haramu kutoka Wizara hiyo, Separatus Fella, alisema zaidi ya washiriki 80 wameshafika katika mkutano wa mafunzo hayo, na matarajio yake makubwa washiriki watapata elimu nzuri kwa ajili ya kupambana na biashara hiyo haramu.
“Mafunzo haya yanatolewa kwa wadau wanaotekeleza sheria ya kuzuia na kupambana na Biashara hiyo, Maafisa Polisi, Uhamiaji, waendesha mashtaka, Mahakimu, Maafisa Ustawi Jamii na Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGO’s) yaliyopo Zanzibar,” alisema Lugola.
Fella alifafanua kuwa, mafunzo hayo yanafanyika kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Marekani linalojihusisha na Masuala ya Utafiti (RTI).
Akizungumza kabla ya kufungua mafunzo ya siku tano ya Watekelezaji wa sheria ya kuzuia biashara hiyo haramu, katika hoteli ya Ngalawa, mjini Unguja, Zanzibar, Lugola amesema wanaofanya kazi hiyo waiache mara moja maana Serikali itawashughulikia.
“Tatizo hili, linaweza onekana likawa dogo, lakini ukweli ni kwamba sote tunafahamu ni kubwa na limeendelea kukua kila mwaka. Uzoefu wa kiutendaji kutoka Sekretareti hususani kutokana na wahanga wanaookolewa unaonyesha kwamba biashara hii inafanyika sana Mkoa wa Dar es Salaam Tanga, Mwanza, Kigoma, Geita, Dodoma, Singida, Arusha, Manyara, Shinyanga na Tanzania Zanzibar,” alisema Lugola.
Lugola alisema licha ya changamoto hizo, lakini Serikali katika kipindi cha kuanzia Januari mpaka Disemba 2018 imefanikiwa kuwaokoa jumla ya Watanzania 147 waliokuwa wahanga wa biashara haramu ya usafirishaji binadamu. Kati ya wahanga 141walikuwa wakitumikishwa katika mikoa mbalimbali nchini.
Pia Lugola alisema wahanga 6 walikuwa wakitumikishwa nje ya nchi ambapo watano walikuokolewa kutoka Thailand na mhanga mmoja kutoka Malasia, na Mhanga mmoja aliokolewa hapa nchini alipokuwa akitumikishwa na taratibu za kumrudisha kwao Msumbiji bado zinafanyika.
“Napenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa hatutamuacha salama mtu yeyote, wanaojihusisha na biashara hii waiache mara moja kabla mkono wa sheria haujawafikia,” alisema Lugola.
Aidha, Lugola alisema Serikali ya Tanzania, haijaikataza Watanzania kufanya kazi nje ya nchi, bali imeweka taratibu zenye lengo za kumlinda Mtanzania na madhara yatokanayo na biashara hiyo haramu.
Kwa upande wake, Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara hiyo Haramu kutoka Wizara hiyo, Separatus Fella, alisema zaidi ya washiriki 80 wameshafika katika mkutano wa mafunzo hayo, na matarajio yake makubwa washiriki watapata elimu nzuri kwa ajili ya kupambana na biashara hiyo haramu.
“Mafunzo haya yanatolewa kwa wadau wanaotekeleza sheria ya kuzuia na kupambana na Biashara hiyo, Maafisa Polisi, Uhamiaji, waendesha mashtaka, Mahakimu, Maafisa Ustawi Jamii na Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGO’s) yaliyopo Zanzibar,” alisema Lugola.
Fella alifafanua kuwa, mafunzo hayo yanafanyika kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Marekani linalojihusisha na Masuala ya Utafiti (RTI).
Siasa Tanzania: Chama cha upinzani ACT-Wazalendo hatarini kufutiwa usajili
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini Tanzania umekipa chama cha ACT-Wazalendo wiki mbili kujitetea kwa
nini wasifutiwe usajili wao wa kudumu.
Wiki moja iliyopita,
kundi la viongozi kutoka chama cha CUF wakiongozwa na Maalim Seif Sharif
Hamad walijiunga na ACT baada ya mgogoro wa muda mrefu wa madarka ndani
ya CUF. Machi 18, Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam ilimthibitisha Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa CUF, hali iliyopelekea Maalim Seif na washirika wake kukihama chama hicho.
Toka hapo, mamia ya wanachama na wafuasi wa CUF hususani katika visiwa vya Zanzibar wamekuwa wakijiunga na ACT, na chama hicho sasa kuonekana ni ngome mpya ya upinzani.
Kwa mujibu wa barua kutoka ofisi ya msajili, vitendo vilivyotokea wakati wa hama hama hiyo ni miongoni mwa sababu za kutoa kusudio la kukifungia chama cha ACT.
"...kumezuka vitendo vya uvunjifuwa Sheria ikiwemokuchoma moto bendera za chama za CUF, vinavyofanywa na mashabiki wa Maalim Seif Sharif Hamad aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, ambao wanadai sasa ni wanachama wa ACT-Wazalendo. Kitendo cha kuchoma moto bendera ya chama cha siasa ni kukiuka kifungu cha 11C cha Sheria ya Vyama vya Siasa," inasema sehemu ya barua hiyo.
Msajili pia amedai kuwa kupitia mitandao ya kijamii, kuna video inayoonesha watu wakipandisha bendera ya ACT kwa kutumia tamko takatifu la dini ya Kiislamu (Takbira). Kitendo hicho, kwa mujibu wa msajili kinavunja vifungu 9(1)(c) na 9(2)(a) vinavyokataza kuchanganya shughuli za vyama vya siasa na dini.
Kwa mujibu wa barua, Machi 19 Msajili alitoa taarifa kwa umma kukemea vitendo hivyo: "Kitendo cha viongozi wa ACT-Wazalendo kutokemea kinaonesha kuwa chama chenu kimeafiki au kilielekeza vitendo hivyo kufanyika," barua ya Msajili imeeleza.Sababu nyengine iliyotajwa na msajili ni ACT kushindwa kuwasilisha ripoti ya hesabu za fedha za chama kwa mwaka 2013/2014.
Utetezi wa ACT-Wazalendo
Kiongozi wa ACT Zitto Kabwe ameiambia BBC Swahili kuwa hoja zote za msajili hazina mashiko na wataandika utetezi rasmi kama walivyotakiwa.
Zitto amesema sheria inawataka kuhakikisha wanachama wao hawavunji sheria na si watu baki, "...kama ilivyoandikwa kwenye barua ya Msajili, wale ambao wamefanya vitendo hivyo si wanachama wetu. Hatuna wajibu nao."Kuhusu taarifa ya ripoti ya hesabu za chama kwa mwaka 2013/2014 Zitto amesema taarifa hizo zilijumuishwa kwenye hesabu za mwaka 2014/2015. "ACT ilianzishwa miezi miwili kabla ya mwaka wa fedha (2014/15) kuisha, hivyo kiuhasibu na kama tulivyoshauriwa na Mkaguzi, tulijumuisha hesabu hizo za miezi miwili katika hesabu za mwaka uliofuatia 2014/2015."
ACT wanatarajiwa kuwa na mkutano wa dharura leo na baadae Zitto ataongea na waandishi wa habari kuanzia saa tano asubuhi.
Ruka ujumbe wa Twitter wa @zittokabwe
TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI*
Kesho tarehe 26 Machi 2019, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe atazungumza na waandishi wa habari.
Muda: Saa tano kamili asubuhi
Mahali: Makao Makuu ya... https://t.co/csTelbbP1U— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) 25 Machi 2019
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @zittokabwe
BBC pia imeongea na mchambuzi wa siasa Tanzania Said Msonga
ambaye amesema ACT kwa sasa inapitia wakati mgumu na kuna uwezekano wa
mambo mawili kutokea, aidaha chama kishindwe kuvumilia vishindo na
kusambaratika ama "kiive na kuwa moja ya nguzo za upinzani nchini. Ni
kama mkate kwenye bekari tu wanaweza kuungua ama kutka wakiwa mkate ulio
bora."Hatua hiyo ya msajili pia imezua mjadala mtandaoni.
Ruka ujumbe wa Twitter wa @JonMrema
Taarifa kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa anatishia kuifuta ACT-Wazalendo ni za kusikitisha, yafaa zikakemewa vikali na kila mpenda demokrasia,Amani, mshikamano na utulivu wa Taifa letu. Msajili ajue kuwa anaweza kulitumbukiza Taifa kwenye machafuko kwa kutimiza hiyo azima yake.— Jon Mrema (@JonMrema) 25 Machi 2019
Pata Habari zaidi na lukwije Entertainment.com
Zimbabwe yagundua uwezekano mkubwa wa kuwa na mafuta na gesi, Rais Mnangagwa afurahia
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa mafuta na gesi asilia kaskazini mwa taifa hilo.
Kampuni ya uchimbaji madini ya Australia kwa jina Invictus Energy kwa ushirikiano na serikali, sasa inatarajiwa kuanza uchimbaji kubaini iwapo mafuta hayo yanaweza kuchimbwa na kuuzwa kibiashara.Kisima cha mafuta kitachimbwa na kampuni ya Invictus katika wilaya ya Muzarabani katika kipindi cha miaka miwili ijayo, rais huyo alisema.
Zimbabwe imekuwa ikishuhudia mgogoro mbaya zaidi wa kiuchumi katika zaidi ya mwongo mmoja.
Imekuwa kawaida kutokea kwa uhaba wa mafuta, na umeme kukatwa.
"Tumeshauriwa na Invictus kwamba matokeo ya upelelezi yana matumaini makubwa na yanaashiria kupatikana kwa mafuta na gesi eneo hilo,2 amesema Mnangagwa.
"Matokeo hayo kama yalivyotangazwa na Invictus ni habari za kufurahisha sana kwa taifa letu."
Waziri wa madini Winston Chitando amesema kisima hicho, ambacho kitachimbwa takriban 240km kaskazini mwa mji mkuu Harare kitachimbwa kwa gharama ya $20m (£15m), kwa mujibu wa sirika la habari la Reuters.
Zimbabwe ina utajiri wa madini mengine lakini haijakuwa na mafuta wala gesi.
Miaka 25 baada ya kampuni ya mafuta ya Mobil kufanya upelelezi wa kutafuta mafuta na kuondoka mikono mitupu, teknolojia mpya inaonekana kuonyesha kuna mafuta kazkazini mwa Zimbabwe, karibu na mpaka wake na Msumbiji.
Upelelezi bado uko katika hatia za awali, lakini serikali ambayo imeishiwa na pesa inaonekana kutaka kutumia habari hizo kufufua matumaini ya wananchi katika taifa lao huku mgogoro wa kiuchumi ukiendelea kuuma.
Raia wamekuwa wakilalamikia kuenea kwa ufisadi na umaskini.
Invictus wanatarajiwa kuchimba kisima katika miaka michache ijayo ndipo ugunduzi wa mafuta hayo uthibitishwe.
Baadaye, itaingia kwenye mkataba wa kugawana mapato na serikali.
Hata kama uchimbaji wa mafuta ya kuuzwa utaendelea, haiwezi kutarajiwa kwamba utajiri huo utafikia kila raia.
Zimbabwe ina madini mengi ya platinum na almasi, lakini manufaa ya mapato yake huwa hayawafikii raia wa kawaida.Hii ni kutokana na ufisadi na sera duni ambazo husababisha baadhi ya madini hayo kusafirishwa nje ya nchi yakiwa bado ghafi.
Chini ya Robert Mugabe, aliyelazimishwa kujiuzulu mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuongoza kwa miaka 37, kulikuwa na mpango wa sera ya kuanzisha viwanda vya madini ndani ya nchi kwa lengo la kuongeza mapato na ajira kwa wenyeji. Lakini hilo halikufua dafu.
Australian who encouraged wife's suicide jailed in landmark case
An Australian man has been sentenced
to 10 years in jail for encouraging his wife's suicide, in a case
believed to have set a global precedent.
Graham Morant, 68, was convicted last month of counselling and aiding his wife, Jennifer Morant, to take her own life in 2014.He had been motivated by a desire to access Mrs Morant's life insurance benefits, a judge ruled.
As sole beneficiary, Morant had stood to receive A$1.4m (£770,000; $1m).
"You counselled your wife to kill herself because you wanted to get your hands on the A$1.4m," Justice Peter Davis said in the Queensland Supreme Court on Friday.
Mrs Morant had suffered from chronic pain, depression and anxiety, but was not terminally ill.
Justice Davis said it appeared to be the first time globally that a person had been sentenced for counselling someone to die by suicide.
'Took advantage of her vulnerability'
Morant had pleaded not guilty to the charges, but a jury found that Mrs Morant would not have ended her life without his counselling.The 56-year-old woman was found dead alongside a petrol generator in her car on 30 November, 2014. Nearby, a note read: "Please don't resuscitate me."
Her husband had previously driven her to a hardware store to buy the generator, the jury was told.
Morant, a devout Christian, had told his wife that he planned to use the insurance money to build a religious commune, according to prosecutors.
On Friday, Justice Davis said Morant had shown no remorse for his offences.
"You took advantage of her vulnerability as a sick and depressed woman," he said.
Morant received a maximum 10-year sentence for the charge of counselling suicide, and a six-year sentence for the charge of aiding suicide. The sentences will be served concurrently.
Mauaji ya Khashoggi: Mwanamfalme wa Saudia anaamini Khashoggi alikuwa mshirika hatari wa kundi la kiislamu. Mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia Arabia mwanamfalme Mohammed bin Salman aliwaambia maafisa wa Marekani kwamba anamchukulia mwanahabari aliyeuawa, Jamal Khashoggi kama mshirika hatari wa kundi la kiislamu lenye itikadi kali.
Mwanamfalme Mohammed ameripotiwa kusema hayo katika mazungumzo yake ya simu na maafisa wa Ikulu ya Marekani baada ya kupotea kwa mwanahabari Jamal Khashoggi.
Saudia hata hivyo imekanusha ripoti hiyo iliyochapishwa katika magazeti ya Washington Post na New York Times.Khashoggi, ni raia wa Saudi Arabia aliyekuwa mchangiaji wa makala maalum katika gazeti la Washington Post.
Alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa kifalme nchini Saudi Arabia.
Mwili haujapatikana
Mwili wa mwanahabari huyo mpaka sasa haujapatikana huku mwendesha mashtaka wa Saudi Arabia akisema mauaji ya Khashoggi yalikuwa yamepangwa.
Huku hayo yakijiri mtoto wa kiume wa Jamal Khashoggi, Salah pamoja na familia yake wamewasili Marekani siku chache baada ya kukutana na Mwanamfalme Mohammed Bin Salman.
Katika taarifa iliyochapisha magazetini familia nya Khashoggi imekanusha madai kwamba Khashoggi alikua mwanachama wa kundi la Muslim Brotherhood.
Familia hiyo pia imeongeza kwamba yeye mwenyewe aliipinga madai hayo mara kadhaa katika miaka ya hivi karibuni.
"Jamal Khashoggi hakua mtu hatari kwa vyovyote. Madai hayo ni ya kushangaza sana," ilisema taarifa hiyo.
Mpaka sasa hakuna makubaliono yaliyofikiwa kuhusu jinsi Khashoggi alivyofariki.
Aliingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul kushughulikia stakabadhi za kumwezesha kumuoa mchumba wake wa Uturuki, Hatice Cengiz.
Siku ya Jumatano Uturuki ilisema kuwa aliuawa alipoingia ndani ya ofisi za ubalozi huo na mwili wake kukatwa katika vipande "kulingana na utaratibu uliopangwa awali''.
Vyombo vya habari vya Uturuki viliwahi kuripoti kuwa Khashoggi aliteswa kabla ya kuuawa.
BREAKING NEWS: Wema Sepetu afikishwa Mahakama ya Kisutu Dar.
Mwigizaji
na mlimbwende wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu amefikishwa
katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018.
Wema
amefikishwa mahakamani hapo saa 4 asubuhi na kupelekwa katika chumba
cha mahabusu kusubiri kusomewa mashtaka ya usambazaji wa picha za
faragha mtandaoni
Amefikishwa mahakamani hapo akisindikizwa na polisi huku akiwa amevaa miwani na kujitanda ushungi.
Mtangazaji wa Star Time TV Afariki Dunia.
Mtangazaji mkongwe wa Star TV na Radio Free Africa za Mwanza, Samadu Hassan, amefariki dunia mjini humo.
Hassan aliyewahi kufanya kazi Kenya na kupata umaarufu mkubwa atakumbukwa kwa uchapaji kazi na sauti maridadi ya utangazaji.
Akizungumza na Mwananchi Digital asubuhi hii, mdogo wa Samadu, Latifa
Hassan amesema kaka yake alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa zaidi ya wiki
moja, kabla ya kufikwa na umauti usiku.
“Samadu alirudi nyumbani kwake jana jioni, akitokea kazini na alikuwa
mzima wa afya, japo alikuwa akilalamika kuwa kifua kilikuwa kinamsumbua
kwa takriban wiki nzima sasa,” amesema Latifa.
“Tulikuwa na maongezi naye kwa muda na baadaye tukala naye chakula hadi
tukamaliza, akatueleza kifua kinamsumbua, tukamshauri pengine twende
hospitali usiku huo kupata matibabu akasema angeenda kesho (leo).”
Hata hivyo anasema ilipofika saa sita kasoro usiku, ghafla hali yake
ilianza kubadilika na alianguka chini na kuanza kutokwa na mapovu
mdomoni.
“Hali hiyo ilitufanya tukimbie kwenda kutafuta gari ili kumuwahisha
hospitali, lakini hadi tumepata gari na kurudi ndani tukakuta tayari
ameshafariki,” amesema Latifa.
Tunatoa pole kwa familia yake, mwajiri wake Sahara Media na waliokuwa wafanyakazi wenzake.
Basi la kutagaa lazinduliwa China.
Basi la kipekee lenye urefu wa mita mbili juu linaloruhusu magari ya kibinafsi kupitia mvunguni mwake limefanyiwa majaribio katika mji waHebei kaskazini mwa Uchina.
Basi hilo linalopigiwa upatu kutatua kabisa tatizo la usafirishaji wa watu katika miji yenye idadi kubwa ya watu ama Transit Elevated Bus (TEB) limefanyiwa majaribio nchini China.Basi hilo linaloendeshwa kwa umeme linauwezo wa kubeba zaidi ya watu 300 .
Basi hilo kubwa lina urefu wa mita 21 na upana wa futi 25 .
Hii ndio mara ya kwanza kwa wabunifu kuonesha basi hilo hadharani baada ya video yake kuvuja katika mitandao mwezi Mei.
Majaribio ya basi hilo la kipekee yalifanyiwa katika barabara iliyofanyiwa ukarabati yenye urefu wa mita 300m.
Basi hilo linauwezo wa kuhudumu kwa kasi ya Kilomita 60 kwa kila saa.
Takriban mabasi hayo manne yanawezwa kuunganishwa na hivyo kuwa na dereva mmoja.
'Mabasi haya ni ya kipekee na moja ya faida yake kuu ni uwezo wake wa
kubeba abiria wengi sana 300 kwa kila basi, pia itaokoa sana nafasi
barabarani'' alisema mhandisi mkuu katika mradi huo mpya wa usafiri Song
Youzhou.
''Inahudumu kama vile treni za kisasa za umeme ila
gharama ya kuwekeza kujenga njia na ukarabati barabarani ikiwemo ujenzi
wa vituo maalum vya TEB ni 1/5 '' Gadget Man Samuel Karumbo: Mwanafunzi aunda gari linalotumia nishati ya jua Kenya.
Mwanafunzi mmoja nchini Kenya ameunda gari linalotumia kawi ya jua, gari ambalo limekuwa likiwavutia watu sana mtaani kwake, na mtandaoni.
Samuel Karumbo, 30, ni mwanafunzi katika chuo cha mafunzo anuwai cha serikali mjini Kitale, Magharibi mwa Kenya lakini ameliunda gari lake katika eneo la Langas, Eldoret si mbali sana na mji wa Kitale.Anasema gari lake, ambalo lina mitambo mitatu ya sola iliyobandikwa, linaweza kusafiri umbali wa kilomita 50 kwa siku.
Karumbo anasema mchana, sola huchukua nishati ya jua na kuibadilisha kuwa umeme ambao unahifadhiwa kwenye betri ambazo ndizo zinazotumiwa moja kwa moja kuliendesha gari hilo na pia wakati jua halijawaka sana.
Gari hilo lina uzani wa kilo 120 na kwenye mteremko hutumia mvuto wa nguvu za ardhi badala ya umeme. Nguvu hutumia tu kwenye kupanda milima au maeneo yenye miinuko.
Bw Karumbo, ambaye jina lake la utani ni Gadget Man, anasema analenga kuwahamasisha watu kutumia kawi safi isiyochafua mazingira.
Gari lake amelipa jina Gadget Man Hybrid Car na upande wa mbele ameandika kwamba ndilo gari la kwanza linalotumia mitambo ya sola Kenya.
Anasema amekuwa na ndoto kuu ya kuwa mmiliki wa gari kwa muda mrefu lakini hakuwa na pesa.
"Sikuwa na pesa za kununua gari lakini niliketi chini na kukumbuka kwamba mimi ni mvumbuzi. Hapo ndipo nilipofikiria wazo la kuunda gari la kipekee, gari linalotumia mitambo ya sola na halihitaji mafuta," anasema.
Aligeuza ubaraza wake kuwa karakana kwa miezi minne na kuligeuza wazo lake hadi kuwa uhalisia.
Anakadiria kwamba ametumia takriban Sh125,000 (dola 1,250 za Marekani) kufanikisha mradi huo.
Bw Karumbo amesomea ufundi wa stima katika chuo hicho cha mafunzo anuwai cha Kitale.
Ameiomba serikali imsaidie kuunda magari zaidi yanayotumia nishati ya jua.
Wakenya mtandao wamekuwa wakimsifu kijana huyo na kuiomba serikali kuunga mkono juhudi zake.
usisahau kutoa maoni pia fatilia habari kilasiku
Zitto Kabwe: Mbunge wa Kigoma Mjini kuomba kuachiliwa huru mahakamani Tanzania.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe, anatarajiwa kuwasilisha ombi la kutaka kuachiliwa huru mahakamani baada yake kulala seli za polisi.
Bw
Kabwe, ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini, ali kamatwana kuzuiliwa na
polisi katika kituo cha polisi Oysterbay kabla ya kuhamishiwa makao
makuu ya polisi kwa mahojiano zaidi. Kufikia jioni, alikuwa anazuiliwa
katika kituo cha polisi cha Mburahati.
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma lilikuwa limemtaka mwanasiasa huyo kuwasilisha vielelezo juu ya kauli aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari Jumapili iliyopita Oktoba 28, 2018.
Mbunge huyo alikuwa amewaambia wanahabari kuwa ana taarifa za wananchi zaidi ya 100 kuuawa katika tukio la mapigano kati ya wananchi wa jamii ya Wanyantuzu na polisi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Alisema hilo lilitokea wakati wa kuwahamisha Wakulima katika eneo la Mpeta wilayani Uvinza mkoani humo.
Masuala ambayo Kabwe alihojiwa kuyahusu
- Mauaji ya polisi na raia katika kijiji cha Mpeta, Uvinza katika mkoa wa Kigoma
- Kutekwa kwa bilionea Mo Dewji
- Hali ya usalama wa taifa Tanzania
- Masuala ya jumla aliyoyaibua wakati wa kikao chake na wanahabari wikendi
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno alisema tuhuma za mbunge huyo hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.
Wakili wa mbunge huyo Jebra Kambole amekiambia kituo chetu cha habari kwamba juhudi zao za kutaka mbunge huyo aachiliwe kwa dhamana ya polisi Jumatano ziligonga mwamba.
"Polisi wameeleza kwamba ... kwa tamko ambalo alilitoa siku ya Jumapili, kuhusiana na hali ya usalama wa nchi, wao wanaamini maneno yaliyotolewa pale ni maneno ya uchochezi na hivyo yanakiuka kifungu cha 55, kifungu kidogo cha (a) cha Sheria ya Makosa ya Jinai Sura 16, ya mwaka 2002," amesema Bw Kambole.
"Kwa msimamo wetu tunaamini kwamba haya ni makosa ya kisiasa, tunaamini kwamba kwa matamko yake aliyoyatoa ni matamko ambayo yanaonesha kutoridhishwa na utendaji wa serikali.
"Kitu ambacho kinaruhusiwa na sheria. Ni maoni ambayo ameyaeleza kama mtu wa kawaida, kama Mtanzania, kama mbunge, ambayo anaruhusiwa kwa mujibu wa sheria, lakini kwa kuwa wao wanafikiri ni kosa, na ndio maana wakati wanaandika maelezo yake, walipofika kutaka kumhusisha na kosa, yeye akasema kama kuna kosa lolote amejuhusisha nalo, ataenda kutoa maelezo ya kina mahakamani."
TRA ilivyogawa makontena ya Paul Makonda.
Leo October 31, 2018 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema tayari makontena RC Makonda yamekwishagawanywa katika mikoa mbalimbali.
“Makontena
takriban 20 yenye Samani zilizokuja kwa jina la Mkuu wa Mkoa wa DSM,
Paul Makonda tumeyagawa katika mikoa mbalimbali baada ya kushindikana
kuyanadi, kwa mujibu wa sheria tunaruhusiwa kuyagawa endapo
itashindikana
Makonda akoleza vita dhidi ya ushoga Tanzania
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul
Makonda ameunda kamati maalum ya watu 17 ili kuhakikisha kuwa watu
wanaofanya biashara chafu za ngono wanachukuliwa hatua za kisheria.
Kamati
hiyo ambayo imejumuisha watu kutoka bodi ya filamu, Mamlaka ya
mawasiliano Tanzania TCRA, polisi kutoka kitengo cha kuzuia uhalifu wa
mitandao,madaktari na wanasaikolojia.Kamati itakayoshughulika na mashoga wanaojitangaza na wasiojitangaza lakini wanajulikana kuwa mashoga.
- Kamati itakawashughulikia wale wote wanaotengeneza picha au video za ngono ambapo mpaka sasa tayari ana udhibitisho wa taarifa za nyumba 24 ambazo zinashughulika na kazi hiyo.
- Kundi ambalo litaangazia watu wote wanaotangaza biashara ya ngono kwa njia ya mtandao ya kijamii kama instagram,whatsapp na facebook.
- Kundi la mwisho ni kundi la watu wanaofanya utapeli kwa njia ya mtandao kwa kutumia majina ya watu wengine vibaya ili kujipatia fedha.
Aidha nyumba zote zinazofanya biashara ya madanguro na kuchua (massage) wahakikishe kuwa wamesajiliwa na wanatumia wataalamu na kama hawafuati utaratibu basi watajulikana kuwa wanafanya biashara ya ngono.
Hata hivyo Makonda amezionya na kutoa angalizo kwa mashirika ya haki za binadamu kuwa Tanzania ina tamaduni zake na ushoga ni kesi ya jinai kwa mujibu wa kifungu cha 154 ambacho kinasema mtu yeyote ambaye anamuingilia mtu yeyote kinyume cha maumbile au, anamuingilia mnyama kimwili au anamruhusu mwanaume kumuingilia yeye mwanaume au mwanamke kinyume cha maumbile,atakuwa ametenda kosa, na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha na wakati mwingine kifungo kisichopungua miaka thelathini .
Tayari nimepokea majina kadhaa ya watu maarufu katika biashara hiyo na
kuna wengine ambao wameeleza kuwa walianza bila kutaka na wanataka kuacha ushoga,
na kuna ambao wanafanya biashara hiyo kwa hiari na kuna wale wanaowekewa vilevi na kufanyishwa biashara hiyo ambao wote watashughulikiwa", Makonda aeleza.
Na mwisho amesisitiza kuwa mapambano haya dhidi ya ushoga na biashara ya ngono sio yake peke yake bali ni ya watu wote .
James 'Whitey' Bulger: Jambazi sugu aliyehusishwa na Mafia Marekani afariki kwa njia ya kushangaza gerezani.
ambazi sugu mjini Boston James "Whitey" Bulger amepatikana akiwa amefariki katika jela moja eneo la West Virginia nchini Marekani.
Jambazi huyo mwenye umri wa miaka 89 alifikishwa katika hospitali ya gereza hilo akiwa tayari ameaga dunia muda mfupi baada ya kuhamishwa kutoka jela la Florida.Afisa wa muungano wa magereza ameliiambia shirika la habari la Associated Press kwamba kifo chake kinachunguzwa kama mauaji.
Maisha ya Bulger, ambaye alifungwa mwaka 2013 baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya watu 11, yaliangaziwa katika filamu kadhaa.
Alikamatwa mjini California mwaka 2011 baada ya kutafutwa kwa miaka 16.
Kiongozi huyo wa zamani wa genge la majambazi wa mji wa Winter Hill kusini mwa Boston aliangaziwa katika filamu ya Black Mass iliyoigizwa na Johnny Depp, na The Departed, ambazo zilishinda tuzo ya Academy kwa picha bora mwaka 2007.
Kifo chake kilitokea siku ambayo alihamishwa katika gereza la Hazelton lililopo West Virginia, ambalo lina wafungwa takribani 1,385.
Vyanzo tofauti vya habari vimeiambia Boston Globe kuwa mfungwa mmoja anayedaiwa kuwa na uhusiano na mafia anachunguzwa kuhusiana na mauaji ya Bulger.
Inasadikiwa kuwa Bulger alishambuliwa vibaya na wafungwa wenzake muda mfupi baada ya kufikishwa katika gereza hilo.
Kwa mujibu wa runinga ya WFXT-TV,mjini Boston, Bulger aliuawa saa kadhaa baada ya kujumishwa na wafungwa wengine.
Wiki iliyopita maafisa wa magereza walikataa kutoa tamko lolote kuhusu hatua ya kumhamisha Bulger ambaye anahudumu kifungo cha maisha katika jela la Florida .
Lakini kwa mujibu wa Globe, Bulger alihamishiwa jela la Florida mwaka 2014 kutoka jela nyingine mjini Arizona baada ya uhusiano wake namshauri wake wa kike kuvutia mamlaka ya magereza.
Maelezo kuhusiana na kifo chake hayajatolewa lakini, maafisa wa magereza wameithibitishia shirika la habari la CBS kwamba kuna tukio la "mauaji" lilitokea Jumanne asubuhi.
"Haya ni mauaji ya tatu katika kipindi cha miezi saba katika gereza hili," Richard Heldreth alisema katika mahojiano ya simu."
Haki miliki ya picha Getty Images Image caption
Taarifa iliyotolewa na idara ya magereza siku ya Jumanne imethibitisha kifo chake akiwa gerezanicustody, na kuongeza kuwa shirika la upelelezi la Marekani,FBI, limeanzisha uchunguzi.
James 'Whitey' Bulger ni nani?
Bulger alizaliwa mwaka 1929 katika familia ya wamarekani wenye asili ya Ireland.
Alilelewa katika kanisa la wakatoliki wa Ireland mjni Boston, ambako alijiunga na genge la Shamrocks, alianza kwa kuiba magari na baadaye akapanda daraja kwa kuingia kaka uhalifu wa kuiba katika benki.
Mara ya kwanza alikamatwa kama kama mhalifu mdogo na hatimaye aliendelea kutawala mamlaka ya uhalifu, kama vile kamari, ulaghai, kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na mauaji.
Baada ya kushtakiwa na kuufungwa kwa kosa la wizi wa mabavu na utekaji nyara alipelekwa katika jela masarufu la Alcatraz katika kisiwa cha San Francisco
Inasemekana aliipenda jela hilo sana kiasi cha kuitembelea akijidai kuwa mtalii wakati alipokua mafichoni.
Hakuna maoni