Header Ads

ad728
  • Breaking News

    Yondani aomba dua za mashabiki

    Yondani aomba dua za mashabiki makundi Shirikisho.

    In Summary.

    By frank lukwije.
    Dar es Salaam. Beki Kelvin Yondani amesema mashabiki wa Yanga wanatakiwa kuwa wamoja ili timu hiyo ifanye vizuri katika hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.
    Yanga imefuzu kwa hatua hiyo kwa mara ya pili, imepangwa kundi D pamoja na timu za USM Alger ya Algeria, Rayons Sports ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya.
    "Hiyo rahisi tu, imekaa sawa kabisa hapo kazi ni kupambana tu  kwa namna ilivyo imani yangu ipo nafasi ya kutengeneza historia nyingine kwa timu, kikubwa wapenzi na mashabiki wa Yanga watuombee Mungu tu," alisema Yondani.
    Alisema, hiyo ni kutokana na namna wanavyojuana, timu kama Gor Mahia na Rayons zote zipo ukanda wa Afrika Mashariki na wamekuwa wakikutana mara kwa mara.
    Endapo Yanga itafanya vizuri hatua hiyo na kusonga robo fainali, itakuwa imeandika historia mpya kwenye soka la Tanzania.


    Hakuna maoni

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728