Header Ads

ad728
  • Breaking News

    #WC2018: Kwa pacha hizi lazima uumie aisee

    #WC2018: Kwa pacha hizi lazima uumie aisee si mchezo mchezo mambo ni hivi(mambo ni moto)

     lukwije Entertainment.com



    ACHANA kabisa na zile kombinesheni zako ulizozoea kuziona pale Real Madrid ya BBC au ile ya MSN ambayo ilibamba kinoma kwa wababe wa Camp Nou, Barcelona. Huko kwenye Kombe la Dunia kuna pacha za hatari kabisa ambazo kama ukikutana nazo ukiwa hujajiandaa basi 5-0 au 3-0 zitakuwa zinakuhusu kabisa.
    Mwanaspoti linakupa pacha hatari ambazo zitasumbua sana kwenye Kombe la Dunia kule Russia huku ile ya Brazil ikionekana kuwa moto kwelikweli.
    Neymar, Gabriel Jesus (Brazil)
    Neymar anafanya kazi yake vizuri sana ya kupasia mpira nyavuni. Huduma yake ndani ya Barcelona iliwafanya PSG wakavunja benki na kulipa pauni 200 milioni kumpeleka jijini Paris. Sasa atakuwa akicheza pamoja na kinda la Manchester City, ambaye huduma yake kwenye kikosi cha Pep Guardiola dio ya kitoto kabisa. Fikiria dogo tu anampiga benchi Kun Aguero! Ndani ya jeshi la Selecao kutakuwa na pacha ya Netmar na Jesus ambao wameiwezesha Brazil kufuzu mapema tu kwenye fainali hizo. Neymar kwa sasa anaendelea kupona majeraha yake, lakini mashabiki wengi sana wanaipa nafasi kubwa Brazil kubeba taji hilo.
    Hazard, Lukaku (Ubelgiji)
    Hawa jamaa wanauwasha moto kwelikweli hapo England na wote panga pangua hawakosi namba kwenye vikosi vyao vya kwanza. Sasa fikiria Hazard na Lukaku wakisimama mbele ya lango la timu pinzani kisha nyuma yao unamkuta fundi wa mpira, Kelvin de Bryune atakayekuwa na kazi ya kupiga pasi za mwisho.
    Kocha Roberto Martinez anakwenda Russia akiwa na imani kubwa kikosi chake kinakwenda kufanya miujiza, japo mara nyingi kimekuwa hakina bahati licha ya kuwa na mastaa wakubwa na wenye viwango bora.
    Griezman na Mbappe (Ufaransa)
    Vijana wa Didier Derchamps wataleta hatari kubwa kule Russia. Wachezaji hawa wanasifika kuwa na kasi, uwezo wa kupiga chenga na kufunga mabao, walikuwa tishio kwenye safu ya ushambuliaji ya Ufaransa katika mechi za kufuzu fainali hizo.
    Isco na David Silva (Hispania)
    Kocha wa Hispania, Julien Lupitegui ameanza kuirudisha Hispania kwenye enzi za utawala wake. Safu ya kiungo ya Hispania inaongozwa na mafundi wa mpira ambao, wanaweza kufanya kitu chochote na wakati wowote na itakuwa moja ya kombinesheni za kutisha kwenye fainali hizo.
    Suarez na Cavani (Uruguay)
    Kombinesheni hii inaitwa weka mbali na watoto. Hawa jamaa wanajua jinsi gani ya kucheka na nyavu, hili linafanya kombinesheni yao kuwa hatari zaidi kwenye lango la timu pinzani.
    Kane na Dele Alli (England)
    Pacha yao inaanzia ndani ya Spurs ambako wamekuwa wakifanya kazi yao vizuri. Alli na Kane wamekuwa wakielewana sana wanapokuwa uwanjani. Wamefanikiwa kutengeneza pacha hatari ndani ya kipindi cha miaka mitatu wakiwa na Spurs na watarajiwa kuhamishia makali yao nchini Russia.
    Kombinesheni nyingine ambazo zitakuwa tishio nchini Russia ni ile ya Luka Modric, Mateo Kovacic na Ivan Rakitic (Croatia), Messi, Higuaín na Di Maria (Argentina), James Rodriguez, Radamel Falcao na Juan Cuadrado (Colombia), Cristiano Ronaldo na Andre Silva (Ureno).
    Imeandaliwa na Frank Lukwije

    Hakuna maoni

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728