Home
/
Unlabelled
/
TRA Wafunguka na Kutoa Ufafanuzi Kuhusu Habari ya “Madudu yaibuka TRA” Iliyochapishwa na Gazeti la Tanzania Daima
TRA Wafunguka na Kutoa Ufafanuzi Kuhusu Habari ya “Madudu yaibuka TRA” Iliyochapishwa na Gazeti la Tanzania Daima
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu habari
zilizochapishwa katika Gazeti la Tanzania Daima la tarehe 26 Oktoba,
2018 toleo namba 4979 na toleo namba 4982 la tarehe 30 Oktoba, 2018
zenye vichwa vya habari “Madudu yaibuka TRA” na “Barua za madudu TRA zavuja”. Habari inayofanana na hizi, ilisambazwa pia katika baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikiwa na kichwa cha habari "PCCB Tanzania, to investigate the two tax collectors TRA and ZRB".
Habari
hizi zinadai kuwa, Mfumo wa Ulipaji Kodi kwa Njia ya Kielektroniki –
Electronic Revenue Collection System (e-RCS) umezimwa na kuhujumiwa na
baadhi ya Maofisa wa Serikali kwa lengo la kujinufaisha na kuzorotesha
juhudi za ukusanyaji mapato ya Serikali.
Ukweli
ni kwamba, mfumo huo haujahujumiwa wala kuzimwa isipokuwa kuna
maboresho ya kiufundi ambayo yanaendelea kufanyika ili kuhakikisha kuwa,
unakidhi malengo yaliyokusudiwa.
Katika
kipindi hiki ambacho maboresho yanaendelea kufanyika, Kampuni za Simu
pamoja na Benki mbalimbali zinaendelea kulipa kodi kwa mujibu wa sheria
na hakuna upotevu wowote wa mapato kama ilivyoripotiwa na Gazeti la
Tanzania Daima na baadhi ya Mitandao ya Kijamii.
TRA
inapenda kuuhakikishia umma kwamba, hakuna Ofisa yeyote wa Serikali
mwenye nia ya kuhujumu mfumo huo kwa lengo la kujinufaisha na
kuzorotesha juhudi za Serikali za ukusanyaji wa mapato.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania inatoa wito kwa vyombo vya habari, wachapishaji,
wahariri na waandishi wa habari kufanya utafiti wa kina kabla ya
kuandika habari na kuzingatia weledi wakati wote wanapotimiza majukumu
yao ili kuepuka upotoshaji.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Imetolewa na:
Richard M. Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI.
Hakuna maoni