Je wajua waweza kujifunza kitu chochote kwa saa 20 tu?
Iwe Kirusi, Kiarabu ama Kichina, au
hata fizikia ya maumbo. Ubongo wa binaadamu unaweza kujifunza kitu
chochote kile, hata kiwe kigumu namna gani, tena kwa haraka.
Utafiti unaonesha kuwa muda bora kabisa wa kujifunza kitu ni saa 20 za awali unapokutana na somo ama ujuzi mpya. Wakati huo ndio kasi ya ubongo kupata uelewa ni kubwa zaidi. Kutokana na hamu ya kung'amua mapya, uwezo wa ubongo kufahamu nao huwa mkubwa.
Mwanafalsafa wa karne ya 19 nchini Ujerumani Herman Ebbinghaus ambaye pia alikuwa ni mwanasaikolojia ni moja ya wasomi wa mwanzo ambao walitafiti juu ya namna ubongo unavyokusanya taarifa mpya.
Kulielezea hilo, Ebbinghaus alitengena kile alichokiita learning curve, yaani mchirizo wa kujifunza: ama uhusiano kati ya kupata stadi mpya na muda utumikao kujifunza.
Mchirizo huo una mihimili miwili wa wima ama y ni wa maarifa na mhimili mlalo ama y ni wa muda.
Ebbinghaus aligundua kuwa kwa saa chache za mwanzo muda mwingi zaidi ukitumika kujifunza somo jipya na ndivyo hivyo maarifa zidi hupatikana.
Lakini baada ya muda kasi ya kujifunza huanza kushuka: japo ukiendelea kujifunza utapata uelewa zaidi lakini si kwa kasi kama ya saa 20 za mwanzo.
Katika wakati huu wa sasa, njia hiyo iliyobuniwa na Ebbinghaus inatumika kama kipimo cha kufahamu muda muafaka wa mtu kujifunza ujuzi mpya, na katika ulimwengu wa biashara hutumika kupima kasi ya utendaji kazi.
Saa 20 za mwanzo ndizo muhimu zaidi kwenye kujifunza kutokana na hamu ya ubongo kuwa juu, lakini kadri ubongo unavyozidi kung'amua somo hilo ndivyo pia unavyochoka na kufanya kasi ya kujifunza kupungua.
Ndio maana hata somo liwe gumu namna gani, athari kubwa zaidi za kuelewa hutokea mwanzoni na kwa haraka kabla kasi kupungua.
Hakuna maoni