Header Ads

ad728
  • Breaking News

    Liverpool 3-1 Manchester United: Upi mustakabali wa Mourinho na Paul Pogba baada ya kichapo?

    Mourinho Kipigo sha goli 3-1 walichokipokea Manchester United mbele ya watani wao wa jadi Liverpool kimewaacha United taabani kwenye msimamo wa ligi hali inayowafanya wachambuzi na wachezaji wa zamani wa klabu hiyo kuchambua mustakabali wa kocha Jose Mourinho na kikosi chake.
    Siku kama ya leo miaka mitatu iliyopita yaani Desemba 17, 2015 Mourinho alifutwa kazi na Chelsea.
    Baada ya kichapo cha jana, wachambuzi wanajiuliza je hatima kama hiyo itajirudia tena hii leo kwa Mourinho?
    "Nadhani hilo litafanyika - japo mie huwa napendelea maamuzi kama hayo yafanyike mwisho wa msimu" mlinzi wa zamani wa timu ya Manchester United, Gary Neville ameiambia Sky Sports. "Lakini ajabu ni kwamba, bodi ya timu haionyeshi kujali kabisa, ni jambo la kusikitisha."
    Ameongeza pia kuwa: "Mara tu [Mourinho] aliporejea kabla ya msimu kuanza, alijikakamua na klabu ilikuwa imedorora. Hakukuwa na mtu juu yake ambaye angeweza kudhibiti klabu. Hawajui kabisa watakalomfanyia, hawana kabisa la kumuambia. Hawajui pia atakachosema, kwenye mkutano na wanahabari. Itatugharimu mno tutakapo mpoteza."

    Siku ya Jumapili, Man United ilicharazwa jumla ya mabao 3-1 katika mechi iliyochezewa uwanjani Anfield, na kuwafanya kuwa katika nafasi ya 6 na alama 19 nyuma ya vinara Liverpool.
    Akizungumzia mchuano huo, mshambulizi wa zamani wa Newcastle na England, Alan Shearer, amesema: "kwa sasa ndani ya kikosi cha Manchester United, ni David de Gea tu ndiye aliye katika nafasi nzuri na bora mno kimichezo.
    "Kuna kitu ambacho lazima kibadilishwa ndani ya klabu hiyo. Bodi ya timu hiyo inatakiwa ichague kati ya kumtimua mkufunzi au kumuunga mkono kwa kumpa fursa ya kuwanunua wachezaji ambao anawataka, kwa sababu kuna mengi ya kufanywa ili kuboresha timu hiyo- kuna ukosefu wa uwezo.
    "Bodi kuu ya timu haijamuunga mkono msimu uliopita, kwa sababu Jose alikuwa na malengo yake na kwa sababu ambayo haijulikani, hawakutakikana kuingilia kati. Lakini sio tu makosa ya mkufunzi- sidhani wengi wa wachezaji wa Man United hapo jana Jumapili walifika wakidhania wamefanya vyema."
    "Ikiwa utafika leo kutoka mwezini na haufahamu lolote kabisa kuhusu soka, utasema Man U ni timu ya kiwango cha wastani katika mchuano wa Ligi kuu ya Premia," amesema nahodha wa zamani wa United, Roy Keane.

      Paul Pogba

     Ni Manchester United ya miaka ya 80, ni timu tu ya kombe la kawaida."

    'Siku za Pogba zinahesabika'

    Paul Pogba alishinda kombe la dunia na taifa lake la Ufaransa mwezi Julai,na alikuwa mchezaji ghali zaidi ulimwenguni baada ya Manchester United kumnunua kutoka Juventus kwa kima cha pauni milioni 89, mwaka 2016.

    Lakini sasa hajachezeshwa mechi tatu mfululizo kwenye ligi.
    Ni mchezaji pekee wa United ambaye wasomaji wa BBC walimchagua kuingia kwenye kikosi bora cha pamoja cha klabu hizo mbili kabla ya mchezo wa jana.
    Je, huu ndio mwisho wa Pogba Old Trafford?
    "Sidhani kama Pogba atasalia kwenye klabu hiyo," amesema mchambuzi na mchezaji wa zamani Roby Savage. "Swali kubwa ni je? Ni nani ataendelea kusalia ndani ya United? Ni Mourinho au Pogba?
    "United wameaibishwa leo (jana) hapa huku Paul Pogba, ambaye kima chake ni Pauni milioni 89, akiwekwa kwenye benchi bila kutumiwa." Keane ameongeza pia kuwa: "Siku za Pogba klabuni zinayoyoma, hawatamuuza mwezi Januari lakini watamuondoa. Sio jambo kubwa, amewahi kuondoka Man U hapo kabla."
    Akihojiwa na Sky Sports, mchezaji wa zamani wa kiungo cha kati wa Liverpool, Graeme Souness amesema: "Nadhani Pogba anawaza akiwazua, mie bila shaka ni bora kuliko Marouane Fellaini, kwa hakika bora kumshinda Nemanja Matic? Lakini ikiwa atabadili mtizamo wake, atakuwa mchezaji wa kiungo cha katio bora zaidi katika michuano ya ligi kuu ya Premia."

     

     

    Hakuna maoni

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728