Godbless Lema Kujiuzulu Ubunge Kama Spika Ndugai Atathibitisha Hili....
Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa endapo Spika wa Bunge Job Ndugai atalithibitishia bunge kuhusu kauli yake dhidi ya matibabu ya Lissu, yeye atakuwa tayari kujiuzulu.
Lema
ametoa kauli hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter ambapo amejibu kauli
iliyotolewa na Spika akiwa bungeni leo ambapo amesema kuwa mpaka sasa
bunge limegharamia shilingi milioni 250 katika matibabu ya mbunge wa
Singida Mashariki Tundu Lissu.
"Bunge
halijawahi kumlipia Mh Lissu pesa kwa ajili ya matibabu, alichokisema
Mh Spika Ndugai ni upotoshaji kwa jamii na Mungu. Chama kitatoa tamko
juu ya hili. Spika akiweza kuthibitisha hili, mimi nitajiuzulu Ubunge,
mshahara wa Mbunge sio hisani ya Spika", ameandika Lema.
Amesema hadi mwishoni mwa Desemba 2018, Lissu alikuwa amelipwa Sh207.8milioni pamoja na Sh43 milioni zilizotolewa kama mchango wa matibabu ya mbunge huyo.
Amesema kwa ujumla hadi sasa Lissu amelipwa Sh250milioni kutoka bungeni.
“Siku za mwanzo sikutaka kujibu maana niliamini kumjibu mtu aliyelala kitandani siyo vizuri kwani kuna vitu huenda vingekuwa vimempita, lakini sasa naamini ni mzima hadi anafanya ziara nje. Nalisema hili akijibu nakuja na mkeka hapa,” amesema Ndugai.
Hakuna maoni