Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 01.02.2019: Cahill, Sarri, Malcom, Hudson-Odoi, Janssen, Austin

Bayern Munich wametupilia mbali mipango ya kumnunua mshambuliaji wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 18, baada ya kutangaza kuwa hawatawasaini wachezaji wengine zaidi msimu huu. (Goal)

Eddie Nketiah atasalia katika uwanja wa Emirates baada ya uhamisho wake kuenda Augsburg kwa mkopo kugonga mwamba. (Football.London)
Mazungumzo kati ya Schalke na Tottenham kumhusu mshambuliaji wa Uholanzi Vincent Janssen, 24 yamegonga mwamba. (Football.London)

Southampton wamekataa ofa ya vilabu vinne vya ligi kuu ya England ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wake Charlie Austin, 29. (Sky Sports)
Udinese wameachana na azma yao ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Derby,Tom Huddlestone, 32. (Derby Telegraph)
Hakuna maoni