Vibaka Wavamia Wodi Ya Wagonjwa katika Hospitali ya Kilimanjaro CRCT mjini Moshi

Watu wawili wanaodaiwa kuwa vibaka, wamevamia kwenye wodi namba moja katika Hospitali ya Kilimanjaro CRCT mjini Moshi na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo simu za mkononi na fedha taslimu.
Watu
 hao ambao inadaiwa walikuwa wawili, waliingia katika hospitali hiyo leo
 alfajiri Machi 25, 2019 majira ya saa 10:00 na kuiba vitu hivyo ambavyo
 ni mali za wagonjwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah amethibitisha kutokea tukio hilo na kudai watu hao wawili ni vibaka.
Akizungumza
 shuhuda wa tukio hilo, Rebeca Msigiti ambaye alikuwa msaidizi wa 
mgonjwa katika wodi hiyo, amesema watu hao ambao ni wanaume, waliingia 
wawili ambapo mmoja alibaki mlangoni na mwingine akaingia ndani na 
kuchukua simu za wagonjwa na mikoba yao.
 
 
 
 
 
 
 
Hakuna maoni