Siasa Zetu Bobi Wine kufanya maandamano Uganda
Mbunge na mwanamuziki nchini Uganda, Robert
Kyagulanyi maarufu, Bobi Wine amesema mapema leo atawasilisha rasmi
barua katika Jeshi la Polisi nchini humo kuwafahamisha kuhusu maandamano
yake ya amani kupinga kuzuiwa vyanzo vyake vya mapato.
Bobi Wine ameeleza kufanya hivyo kufuatia kitendo cha kuzuiwa kufanya
tamasha lake kwa madai kwamba hawakuwa na uwezo kudhibiti maelfu ya
mashabiki wake.Amesema Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni anataka kuwazuia wanamuziki wote ambao hawamuungi mkono.
‘Rais Museveni amewaagiza Polisi kuzuia matamasha yangu kwa sababu hapendi kusikia ninachokiimba. Alitaka mimi niwe kama baadhi ya wasanii wanaoimba nyimbo za kumsifu na nilipokataa akaamua kuwa hataniruhusu kufanya onyesho lolote la muziki wangu nchini Uganda,’’ amesema Bobi Wine.
Msanii huyo ambaye pia ni mbunge wa upinzani, alikamatwa jana na kuzuiwa kwa saa kadhaa baada ya kupanga kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ya Serikali kumzuia kufanya tamasha lake la Pasaka
Hakuna maoni