Hakimu Aagiza Wafuasi 18 wa CHADEMA Wasakwe
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuwasomea maelezo ya awali (PH) washtakiwa 31 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema kutokana na washtakiwa wengine 18 kutofika mahakamani.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na shtaka moja la kufanya mkusanyiko usio halali.
Wakili
wa Serikali, Faraji Nguka alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Agustin Rwizile
kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusoma maelezo ya awali (PH) lakini
kuna washtakiwa ambao waliomba hati za kuwakamata na bado wanaendelea
kuwatafuta.
"Tupo
tayari kuendelea na hoja za awali licha ya wafuasi 18 kutokuwepo
mahakamani, tulishaomba hati za kuwakamata bado tunaendelea kuwatafuta,"
amedai Faraji Nguka.
Wakili
wa kujitegemea, Majura Magafu amedai kwa mujibu wa sheria ya makosa ya
jinai, huwezi kuendelea kama mshtakiwa hayupo mahakamani bila taarifa
yoyote ya maandishi.
"Kesi
inaruhusiwa kuendelea bila kuwakilishwa kama mshtakiwa atakuwa
amewasiliana na wakili wake na kumpa taarifa tena kwa njia ya maandishi"
amedai Wakili Magafu.
Wakili
wa Utetezi, Alex Massaba amedai licha ya mahakama kutoa hati za
kuwakamata washtakiwa, kumekuwa hakuna jitihada zozote za kuwatafuta.
Baada
ya maelezo hayo Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 17,mwaka
huu kwa ajili ya kutolea uamuzi kama kesi hiyo iendelee na hoja za
awali.
Hakuna maoni