Viungo wote Man United wakali
Na katika michezo, lukwije Entertaiment.com inakuletea taarifa za moja kwa moja kutoka uwanjani.
In
Summary
Mpango huo wa
kunasa kiungo wa kati umedaiwa hauhusiani kabisa na hatima ya Paul Pogba hasa
baada ya Kocha Jose Mourinho kuhitaji kuendelea kuwa na huduma ya staa huyo wa
Ufaransa ili kikosi chake kiwe na uwezo wa kumiliki mpira na kupangua ngome
ngumu za wapinzani.
MANCHESTER
United wapo siriazi katika mpango wao wa kusajili kiungo wa kati katika dirisha
lijalo la uhamisho wa wachezaji kwenye majira ya kiangazi.
Mpango
huo wa kunasa kiungo wa kati umedaiwa hauhusiani kabisa na hatima ya Paul Pogba
hasa baada ya Kocha Jose Mourinho kuhitaji kuendelea kuwa na huduma ya staa
huyo wa Ufaransa ili kikosi chake kiwe na uwezo wa kumiliki mpira na kupangua
ngome ngumu za wapinzani.
Staa
wa Real Madrid na Ujerumani, Toni Kroos ndiye anashika namba moja kwenye ile
orodha inayosakwa na Mourinho, lakini wasiwasi mkubwa uliopo ni kama Los
Blancos watakubali kumpiga bei staa huyo.
Kutokana
na hilo, Mourinho ameweka bayana orodha ya viungo wengine wakati anaotaka
kusajili kama atakwama kwenye mpango wake wa kumnyakua Kroos.
Viungo
anaowataka Mourinho kwenye orodha yake, yupo staa wa Napoli, Jorginho, kiungo
Fred wa Shakhtar Donetsk’s Fred, Julian Weigl wa Borussia Dortmund na Carlos
Soler wa Valencia.
Yeyote
kati ya viungo hao ataifanya Man United kuwa na ufundi mwingi katikati ya
kiwango na ndiyo maana Mourinho anahaha usiku na mchana kupata huduma zao na
hilo linaweza kuwezekana kutokana na pesa ndefu waliyon.
Hakuna maoni