Bilionea mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha athibitishwa kufariki dunia ajali ya helikopta Uingereza
Bilionea mmiliki wa klabu ya
Leicester City FC amethibitishwa kuwa miongoni mwa watu waliofariki
katika ajali ya helikopta karibu na uwanja wa klabu hiyo Jumamosi.
Klabu
hiyo imethibitisha kuwa Vichai Srivaddhanaprabha, 61, kutoka Thailand,
wafanyakazi wawili wake, rubani na abiria mmoja walifariki baada ya
ndege hiyo kuanguka mwendo wa saa mbili unusu usiku.Bilionea Mmarekani David Rockefeller afariki
Mambo matano unayoyahitaji kuwa bilionea
Walioshuhudia wanasema ndege hiyo ilikuwa tu imemaliza kuondoka uwanjani pale ilipoanza kuyumba na kuanguka na kuwaka moto.
Maelfu ya watu wameweka maua na skafu za ukumbusho nje ya uwanja wa King Power, na pia ujumbe wa kuwafariji waliofiwa.
Polisi wa Leicestershire wamesema waliofariki duniani wanaaminika kuwa:
- Mmiliki wa Leicester Vichai Srivaddhanaprabha
- Wafanyakazi wake wawili, Nursara Suknamai na Kaveporn Punpare
- Rubani Eric Swaffer na mpenzi wake Izabela Roza Lechowicz
Bi Swaffer alikuwa na uzoefu wa miaka 20 akiendesha ndege za kibinafsi na helikopta.
Katika taaluma yake, alikuwa ameendesha helikopta zinazotumiwa na vyombo vya habari kufanya matangazo ya moja kwa moja.
Miongoni mwa mashirika aliyoyafanyia kazi ni Channel 4 katika kipindi chao cha The Big Breakfast na pia amewafi kufanyia kazi kipindi cha Virgin Radio.
Lucie Morris-Marr, rafiki yake Swafer, amesema alikuwa rubani mzoefu sana na bila shaka angefanya kila aliwezalo kuzuia ajali hiyo.
- Utata kuhusu kifo cha bilionea na mke wake Canada
- Mo Dewji: Polisi Tanzania wanasema watekaji walitaka pesa
- Utata waibuka gari alilotekewa Mo Dewji
"Sio watu wengi huamka na kusafiri na wapenzi wao, wakisafiri maeneo mbalimbali duniani na baadhi ya kifahari," alisema.
Wawili hao wapenzi walikuwa marubani na walikuwa wakiishi pamoja Camberley, Surrey.
Bi Lechowicz alihamia Uingereza kutoka Poland 1997.
Hakuna maoni