Mwanafunzi aliyejilipia ada ya masomo kwa kumtengenezea Lil Wayne mkufu.
Mwanafunzi wa sanaa ambaye
alitengeneza mkufu wa dhahabu kwa mwanamuziki Lil Wayne amesema mauzo
yake yalimsaidia kulipa karo yake ya chuo kikuu.
Joy
Bonfield-Colombara, 29, kutoka kusini mashariki mwa London, alisema
alikuwa na wakati mgumu kulipa karo ya pauni 9,500 kwa mwaka kwenye chuo
cha sanaa cha Royal College of Art.Lakini wakati akitathmini kuacha masomo, alipata ujumbe wa barua pepa kutoka kwa rafiki wa rapa huyo raia wa Marekani, ambaye alikuwa anataka kumnunulia mkufu huo kama zawadi ya siku ya kuzaliwa.
Mkufu huo wa dhahabu una uso wa Lil Wayne.
Wanamuziki watano wa Hip Hop matajiri zaidi duniani
Albamu ya hivi majuzi ya Lil Wayne ya Tha Carter V, inayowashirikisha wanamuziki Snoop Dogg, Nicki Minaj, Travis Scott na Kendrick Lamar, ilishika namba tano katika jadwali la muziki nchini Uingereza mwezi huu.
Bi Bonfield-Colombara, ambaye pia anafahamika kama Joy BC, alishangaa sana wakati alijulishwa kiwango cha pesa ambacho angelipwa alichosema ni maelfu kadhaa wa pauni.
Alisema alikuwa na muda wa wiki mbili hadi tatu kumaliza kazi hiyo kabla ya siku ya kuzaliwa ya miaka 36 ya Lil Wayne.
"Nilimpigia mpenzi wangu simu na kumuambia nimeshangazwa sana," alisema.
"Nilichonga kila kitu kwa mikono yangu, hunichukua muda mrefu sana. Mkufu mmoja nilimtengenezea mtu ulinichukua miezi 9.
"Mpenzi wangu aliniambia nisitengeneze sawa na wa Ronaldo," alisema. Akimaanisa sanamu ya Ronaldo iliyokosolewa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Bi Bonfield-Colombara, ambaye aliwai kusomea Glasgow School of Art, alisema amekuwa akituma maombi ya msaada kwa masomo yake.
"Mama yangu alichukua mkopo wa benki na mimi nikapata mkono wa serikali, kwa mahitaji yangu nilitegemea karo yan
Hakuna maoni