Brexit: Baraza la mawaziri Uingereza laidhinisha rasimu ya makubaliano ya kujitoa katika EU
Brexit: Baraza la mawaziri Uingereza laidhinisha rasimu ya makubaliano ya kujitoa katika EU.
Baraza la Mawaziri nchini Uingereza
hatimaye limeidhinisha rasimu ya mswada wa makubaliano juu ya nchi hiyo
kujiondoa katika Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya majadiliano makali yaliyoduymu kwa takriban saa tano,Bi May amesema kwamba atawasilisha taarifa hiyo leo katika bunge la nchi hiyo, ambapo ataelezea uamuzi wa serikali.
Amekuwa mbioni kutetea mapendekezo ya mkataba baina ya Uingereza na muungano wa ulaya unaohusu masharti ya jinsi Uingereza itakavyoweza kujiondoa katika muungano huo.
Wafuasi wenye msimamo mkali wanaounga mkono Uingereza kujitoa kwenye muungano huo wanadai kuwa mkataba huo ni sawa na kusalimu amri.
Wamekuwa wakitoa wito wa kura kupigwa tena ili kuamua kama Uingereze ijitoe au kusalia kwenye muungano huo.
May pia amesisitiza bungeni kuwa Uingereza itajitoa kwenye muungano wa Ulaya.
"tuko katika hatua ya mgawanyiko" lakini mchakato wa Brexit,unaendelea na utatoa nafasi ya makubaliano hayo kukamilishwa.
Mpatanishi mkuu wa Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya Brexit Michel Barnier amesema mswada huo wa makubaliano umewasilisha hatua ya maamuzi katika majadiliano, lakini bado kuna kazi ya kufanya.
Lakini Jacob Rees-Mogg mmoja wa viongozi wakuu wanaotaka Uingereza kujiondo kwenye muungano wa EU ameutaja mswada huo kama "mkataba uliyooza".
Mhariri wa BBC wa siasa za Uingereza Laura Kuenssberg amesema ni wazi kuwa baraza la mawaziri ''halikuzungumza kwa kauli moja'' huku mawaziri tisa wakiupinga mkataba huo wazi wazi
Hakuna maoni