Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 15.11.2018
Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 15.11.2018: De Gea, Wenger, Foden, Neymar, Mbappe, Smalling.
Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene
Wenger amekataa kuchukua nafasi ya Slavisa Jokanovic kuwa kocha wa
Fulham ingawa tayari Claudio Ranieri alikuwa amepewa. (Daily Mirror)
Huku
meneja wa zamani wa Chelsea na Tottenham, Andre Villas-Boas pamoja na
kocha wa zamani wa Monaco Leonardo Jardim wote wameikataa nafasi ya
kuiongoza Fulham. (Telegraph)Meneja mpya wa Fulham Ranieri, anataka kumsajili mlinzi wa Liverpool Joel Matip, 27 mwezi Januari. (A Spor, via Talksport)
Real Madrid iko tayari kumchukua mmoja wa washambuliaji wa Paris St-Germain kama klabu ya Ufaransa itawauza wachezaji wake kutokana na sababu za matumizi zaidi ya kifedha. Wachezaji hao ni Neymar, 26, na Kylian Mbappe, 19. (AS - in Spanish)
Fifa inavichunguza vilabu vitano vya ligi ya England kuhusu uvunjwaji wa kanuni za usajili wa wachezaji wa kigeni ambao wako chini ya umri wa miaka 18.
Timu hizo zitafugiwa kufanya usajili ikiwa zitakutwa na hatia ya kukiukwa na kanuni za usajili. (Daily Telegraph)
Everton inataka kumsajili mlinzi wa kati Chris Smalling, 28,mwishoni mwa msimu huu wakati ambao mkataba wake utakuwa umeisha. (The Sun)
Kiungo wa kati wa Manchester City na England Phil Foden,18 anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka sita. (Daily Telegraph)
Chelsea wanavutiwa kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund Christian Pulisic, 20, katika msimu wa kiangazi. (The Guardian)
Chelsea wako tayari kusikiliza ofa ya mkopo ya mlinzi wa kati na nahodha Gary Cahill, 32, ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu. (Daily Mail)
Wolves inatamani kumsajili mlinzi wa Argentina Marcos Rojo, 28, ambaye atakuwa huru kuondoka Manchester United mwezi Januari. (Birmingham Mail)
Newcastle inavutiwa na Miguel Almiron mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni kiungo wa kati wa Paraguay anayecheza ligi ya nchini Marekani. (The Chronicle)
Hakuna maoni