Header Ads

ad728
  • Breaking News

    CCM Wazidi Kumkomalia Benard Membe....Katibu Mkuu Agoma Kujibu Jumbe zake za Mitandaoni

     

     Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amekataa masharti yaliyotolewa na kada wa chama hicho, Bernad Membe katika ujumbe wake kupitia kitandao ya kijamii na kusema huo siyo utaratibu wa kukutana na wanachama wake.

    Dk Bashiru amesema hayo leo Jumamosi Desemba 1, 2018 wakati akizungumza na wajumbe wa  mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

    Amesema katika miaka 10 iliyopita CCM haikufanya vizuri kutokana kikundi cha wachache kujifanya ndiyo wenye nguvu na kudharau jambo lililosababisha chama kisipendwe na wapiga kura.

    Amesema tangu achaguliwe kuwa katibu mkuu hajawahi kuonana na Membe na licha ya chaguzi zote zinazofanyika za kurudisha wabunge, Membe aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje hajawahi kutoa mchango wowote wa mawazo.

    Amesema Membe kama mwanachama mwingine hana nguvu zaidi ya chama hivyo bado anamhitaji afike kwake bila masharti yoyote.

    "Sikumsema Membe kama mtu maarufu au mwenye nguvu bali nimemsema kama mwanachama wa kawaida, hana tofauti kabisa na wanachama walioingia leo, ila ana tofauti kwa kuwa amekuwa waziri na mbunge” amesema Dk Bashiru

    “Namuhitaji sana (Membe), ningekuwa na namba yake ya simu ningempigia,” ameongeza.

    Hakuna maoni

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728