Joshua Nassary "Apewa Makavu" Mbele ya Rais Magufuli
Mbunge
wa Viti Maalum CCM, Amina Mollel amedai tangu Joshua Nassari
alipochaguliwa kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema,
ametokomea kusikojulikana na hajui shida za wananchi waliomchagua.
Mollel
ametoa madai hayo leo Jumapili Desemba 2, 2018 katika uzinduzi wa mradi
wa uboreshaji huduma za maji safi na maji taka katika jimbo la Arumeru
Mashariki uliofanywa na Rais Magufuli.
"Naamini
walifanya makosa na hawatarudia tena 2020 na mimi niko hapa kwa ajili
ya kuwasemea ili kuhakikisha shida zao zinatatuliwa," amesema Mollel.
Katika uzinduzi huo Nassari hakuwepo.
Hata
hivyo, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa
Chadema, John Mrema alisema Nassari yupo na wananchi wake na anafanya
shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwamo katika sekta ya elimu na afya.
“Kuna
kipindi Nasari alikuwa anasoma ila kwa sasa amemaliza na anaendelea na
shughuli zake za Kibunge, Amina si msemaji wa wananchi wa Arumeru kazi
hiyo ni ya wananchi wa Arumeru na kama alitaka kushitaki angewashitaki
kwa Rais, mawaziri waliotajwa kutohudhuria vikao vya Bunge.
Kwa
upande wake mbunge wa Monduli, Julius Kalanga amemuomba Rais kuwasaidia
kuondokana na shida ya maji kwa sababu wananchi wake wana hali mbaya.
Amesema hata akipewa nafasi kadhaa za kutoa maombi yake ili aweze kusaidiwa katika utekelezaji mara zote angetaja maji.
"Kama
ulivyowakumbuka wenzetu wa Arumeru, tunaomba na sisi utukumbuke katika
ufalme wako kwa sababu tuna shida kubwa ya maji," amesema Kalanga.
Hakuna maoni