Tetesi za soka Jumanne 04.12.2018: Pulisic, Diaz, Ramsey, Loftus-Cheek, Hernandez, Fabregas
Tetesi za soka Jumanne 04.12.2018: Pulisic, Diaz, Ramsey, Loftus-Cheek, Hernandez, Fabregas.
Chelsea kwa mara ya kwanza
imewasiliana rasmi na Borussia Dortmund kuhusu nia yao ya kutaka
kumsajili winga wa Marekani Christian Pulisic, lakini huenda klabu hiyo
ya Ujerumai ikaitisha euro milioni 70 ili kumuachia mchezaji huyo mwenye
miaka 20 ambaye anapania kujiunga na klabu ya Liverpool. (Evening
Standard)
Kiungo wa kati wa Uhispania Brahim Diaz, 19, anajiandaa
kuondoka Manchester City na kujiunga na Real Madrid, licha ya ombi la
Pep Guardiola la kumtaka asalie katika klabu hiyot. (Sun)Meneja wa Arsenal Unai Emery anasema kuimarika kwa kiwango cha Aaron Ramsey ni jambo jema kwa kiungo huyo wa Wales wa na kwamba uamuzi wa klabu hiyo ni kutoweka wazi kandarasi yake.
Vilabu vya Crystal Palace, Bournemouth, West Ham, Newcastle vinavyoshiriki ligi ya primia pamoja na Schalke ya Ujerumani vinapania kumsajili kiungo wa kimataifa Ruben Loftus-Cheek, 22, anayechezea klabu ya Chelsea baada ya kiungo huyo kukiri kuwa hali ni ''ngumu'' kutokana na kutopangwa katika kikosi cha kwanza. (Mirror)
Mshambuliaji wa West Ham na Mexico Javier Hernandez, 30, ana mpango wa kuhama klabu hiyo mwezi ujao.
Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas anaweza kuondoka bila malipo msimu ujao na pia anaweza kujadili kandarasi nyingine na klabu ya ughaibuni.
Ajenti wa mwenye asili ya Hispania anadaiwa kukutana na AC Milan, ambao wanammezea mate mshambulizi wa zamani wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, 37. (Football Italia, via Sun)
Hakuna maoni