Header Ads

ad728
  • Breaking News

    Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 05.12.2018: Pogba, Hasenhuttl, Gomes, Fabinho, Ibrahimovic.

    Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 05.12.2018: Pogba, Hasenhuttl, Gomes, Fabinho, Ibrahimovic.

     Paul Pogba

    Juventus wanatafakari kuweka dau ya kumnunua Paul Pogba 25, kiungo wa kati wa Manchester United na timu ya Taifa ya Ufaransa. (Sun)
    Southampton wanatajia kukamilisha shughuli ya kumuajiri meneja wao mpya Ralph Hasenhuttl kutoka RB Leipzig kabla ya mechi ya Jumatano dhidi ya Tottenham. (Guardian)
    Kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes anayechezea klabu ya Everton kwa mkopo hajaonesha nia ya kutaka kurudi Barcelona.

    Everton sasa inapania kutumia uamuzi wa kiungo huyo wa miaka 25 kuimarisha dau lake kwa lengo la kupampatia mkataba wa kudumu. (Times)
    Kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Fabinho, 25, amesema haoni sababu ya yeye kujiunga na Paris St-Germain mwezi Januari mwakani licha tetesi kuwa huanda akahamia klabu hiyo ya Ufaransa. (UOL, via FourFourTwo)
    Mshambuliaji wa LA Galaxy na Sweden wakati mmoja Zlatan Ibrahimovic, 37, huenda akarejea AC Milan hivi karibuni.(Goal)




    Zlatan Ibrahimovic
    Manchester City huenda ikamnunua winga wa Leeds United Jack Clarke 18, mwezi January. (Sun)
    Meneja wa Monaco Thierry Henry anataka kumsajili mshambuliaji wa Italia Stefano Okaka, 29 ambaye hana raha tena ya kusalia Vicarage Road. (Mirror)
    Fulham,Crystal Palace na West Ham wanafuatilia mchezo wa mshambuliaji wa Nantes na Argentina Emiliano Sala, 28. (Mirror)

    Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amekataa kuidokezea kituo cha habari cha Klabu hiyo MUTV, kikosi kitakacho Menyana na na mahasimu wao wa jadi Arsenal. (Mail)
    Arsenal ina matumaini ya kuwashinda Bayern Munich na Barcelona katika kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe kutoka Lille.


    Nicolas Peperystal Palace na Newcastle pia wanamfuatilia kwa karibu mlinzi wa Real Betis na Uhispania Junior Firpo 22.(Sun)
    Kiungo wa kati wa zamani wa England na Liverpool Gerrard anasema hatua ya kuongoza Rangers imemsaidia kujiamini zaidi baada ya kustaafu kutoka uwanjani. (Telegraph)
    Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anatafakari mahali hatua yake ya baadae anapojiandaa kwa msimu ujao wa uhamisho mwezi Januari. (Mirror)
     Cesar Azpilicueta

    Hakuna maoni

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728