Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 04.02.2019: Silva, Lennon, Krkic, Diaz, Balotelli, Silva, Real Madrid
Mshambuliaji wa Marseille Mario
Balotelli, 28, anasema kuwa anataka kumaliza kazi yake ya kusakata soka
kwa kuichezea timu yake ya nyumbani ya Brescia nchini Itali. (goal)
Mkufunzi
wa Everton Marco Silva anasema kuwa anajua kwamba yuko chini ya
shinikizo baada ya kikosi chake kushindwa na klabu ya Wolves na kusalia
katika nafasi ya tisa katika jedwali la ligi ya Uingereza. (mirror)Klabu ya Leeds inataka kumnunua winga wake wa zamani Aaron lennon, 31, kurudi katika klabu hiyo kwa kupitia kumsajili kutoka klabu ya Burnley mwisho wa msimu huu. (sun)
Mshambuliaji wa Stoke City Bojan Krkic ,28, huenda akahamia katika klabu ya ligi ya Marekani New England Revolution ambayo imejitolea kumlipa mara mbili marupurupu yake huku dirisha la uhamisho nchini Marekani likiendelea kuwa wazi hadi tarehe mosi mwezi Mei. (sun)
Real Madrid haitamuuza kwa mkopo mwisho wa msimu huu kiungo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 19 kinda Ibrahim Diaz ambaye walimsajili kutoka Manchester City. (AS)
Shirikisho la soka la Uingereza FA linataka kuanzisha refa wa kwanza atakayesimamia mechi za ligi ya wanawake ya.. (telegraph).
Kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21, huenda akaitwa na timu ya Uingereza ilio na wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 baada ya kushirikishwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.(Chronicle).
Hakuna maoni