MBINU 10 ZA KUPUNGUZA MWILI WAKO KWA HARAKA
Ukiwa na mwili unaoupenda kunakufanya ujiamini na uwe na
furaha, na hivyo kujifungulia fursa nyingi katika maisha yako. Kuna msemo
unasema :” When you look good, you feel good, and when you feel good, you do good”
Yaani kama ukionekana vizuri, utajisikia vizuri, ukijisikia vizuri, utafanya
mambo mazuri.
Hivyo inapofikia hatua mtu hufurahii uzito na ukubwa wa
mwili wako, bila shaka unahitaji kuchukua hatua ya ziada ili kuudhibiti huo
mwili na kuurudisha katika muonekano unaoutaka wewe. Kama upo katika hali hiyo
basi usikate tamaa na kujichukia. Bado unayo nafasi ya kuutengeneza mwili wako
vile utakavyo.
Leo nikueleze mbinu 10 ambazo watu wengi wamezitumia na
zimeonyesha mafanikio makubwa katika kupunguza mwili. Njia hizi ni salama na za
haraka kama ukifuata kwa uhakika kama inavyoshauriwa.
Kupungua mwili kunaaanza kwa jinsi vile ulivyo weka
kipaumbele wa swala zima. Unahitaji kupanga muda haswa na kujituma ili ufikie
kuutengeneza mwili wako vile utakavyo.
Muhimu kuzingatia:
Kabla haujanza mpango huu wa kupunguza uzito unapaswa kujua
una kilo ngapi na lengo lako unapaswa kuwa na kilo ngapi na baada ya
muda gani.
Kupanga muda sahihi kunakusaidia kuweka malengo ya kwamba ndani ya kipindi gani au muda gani unataka uwe umepunguza kilo ngapi. Kwa mfano unaweza weka kwamba ndani ya mwezi mmoja uwe umepungua kilo 10.Kwenye mwezi mmoja unaweza weka malengo kila wiki unapungua kilo 3 .
Ninaposema kilo 3 maana yake unaweza kutimiza hicho kiwango au kupunguza zaidi ukawa chini ya kiwango.
Kupanga muda sahihi kunakusaidia kuweka malengo ya kwamba ndani ya kipindi gani au muda gani unataka uwe umepunguza kilo ngapi. Kwa mfano unaweza weka kwamba ndani ya mwezi mmoja uwe umepungua kilo 10.Kwenye mwezi mmoja unaweza weka malengo kila wiki unapungua kilo 3 .
Ninaposema kilo 3 maana yake unaweza kutimiza hicho kiwango au kupunguza zaidi ukawa chini ya kiwango.
Mbinu sahihi za
kufuata ili kuweza kupunguza uzito.
1) Tambua mahitaji ya Calories (karolis) kwenye mwili wako:
Carolies ni neno la kitaalam linalomanisha kiasi cha nguvu
(energy) inayoingia au unayoitoa kuitoa katika mwili wako. Watu tofauti tofauti
huwa na mahitaji tofauti ya calories. Fanya mpango umuone mtaalamu wa lishe
akusaidie ujue kiwango halisi cha calories unachohitaji kuingiza kwa siku na
kiasi gani unatakiwa kutoa kwa siku.
Kutoa au kupunguza calories unatakiwa ufanye mazoezi madogo madogo na pia uwe makini na calories unazoingiza.
Kutoa au kupunguza calories unatakiwa ufanye mazoezi madogo madogo na pia uwe makini na calories unazoingiza.
2) Matumizi ya
matunda na mboga za majani kwa wingi zaidi.
3)Punguza kiwango cha chakula .kupunguza kiwango
cha chakula maana yake kama ulikuwa unakula sahani 2 kwa mlo au chakula
kilichokingi basi punguza sana sana sahani moja tuu.
4)Tumia nyama nyeupe kwa wingi na zilizoiva vizuri zaidi.
5)Usithibiti sana vyakula unaweza kula vyakula uvipendavyo
lakini kwa kiwango kidogo sana.kama nyama ,chips, chocolate
6)Epuka sana matumiz ya soda , bia na juice za
viwandani.badala yake tumia juice za asili ukiepuka sukari.
7)Maji yafanye kuwa sehemu ya maisha yako na unywaji
mwingi wa maji kuna kusaidia kutokuwa na njaa za mara kwa mara. Na unashauriwa
kunywa maji nusu saa kabla ya kula na baada ya kula.
8) Epuka kula chakula na kwenda kulala au kukaa sehemu moja.
Baada ya kula chakula unashauriwa kufanya kazi kidogo ili chakula
kiweze kupungua.
9) Kwa wale wenye magari punguza matumizi ya gari zaidi
tumia mda mwengine kutembea umbali mfupi . Asilimia kubwa ya watu wa mjini
wanakuwa wanene kwa matumizi ya magari na bodaboda na bajaji mwili
unakuwa haupati zoezi au kuchangamka.Jitahidi kutembea umbali mfupi kwa Afya
zaidi.
10) Kuwa na heshima na mwili wako na kuwa makini na
kila ambacho unaingiza kwenye mwili wako . Punguza msongo wa mawazo kwani
inaweza athiri tabia yako ya ulaji , ukajikuta unakula sana na bila mpangilio.
Kutaka kupunguza mwili kuna kuja na nidhamu ya yako ya
kuheshimu matakwa ya mwili wako kuwa bora na kutoka hatua moja kwenda
nyingine.
Share It —
Hakuna maoni