Umoja wa mataifa waingilia sakata la IAAF kutaka kumtenga mwanariadha Caster Semanya kuhusu jinsia yake
Mipango ya kuwatenga wanariadha wa kike kulingana na viwango vyao homoni
za testosterone “Ni ukiukaji wa haki Kimataifa za biadamu ” linasema
Baraza la haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.
Mshindi wa mbio za Olympic mita 800 Caster Semenya, mwenye umri wa miaka 28, anapinga nia ya Shirikisho la kimataifa la Riadha (IAAF) juu ya mpango kuweka masharti ya viwango vya testosterone miongoni mwa wanariadha wa kike.
Umoja wa mataifa imeitaja mipango hiyo kama “isiyo na umuhimu , ya udhalilishajia na yenye mathara “. IAAF imesema kuwa muswada uliopatiwa Umoja wa Mataifa unajumuisha “kauli zisizo sahihi”.
Umoja wa Mataifa wazitaka bodi za michezo kuacha kuandaa na kutekeleza sera zinazowasukuma wanariadha wanawake na wasichana kupitia tiba zisizo za lazima
Chini ya sheria za IAAF, mwanariadha wa kike mwenye viwango asilia vya juu vya homoni za testosterone anatakiwa kukimbia na wanaume au kushiriki mashindano ya watu waliobadilishwa mpaka apate tiba ya kupunguza viwango hivyo.
Sheria hizo zinawahusu wanawake wanaokimbia mbio za mita 400 na maili moja na inawapasa wanariadha hao kuhakikisha viwango vya testosterone vinakuwa chini kulingana na kiwango kilichowekwa. “kwa walau miezi sita kabla ya mashindano “.
Suala hilo lilijadiliwa na kikao cha 40 cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa cha mwezi Machi, ambapo wajumbe waliomba ripoti yenye maelezo ya kina juu ya suala hilo iandaliwe kwa ajili ya mkutano ujao.
Kabla ya hayo, baraza hilo lilielezea “hofu zake ” juu ya mapendekezo ya IAAF. Baraza hilo limesema bodi za utawala hazinabudi “kuacha kuandaa na kutekeleza sera na utendaji ambao unalazimisha , kushurutisha au kuwasukuma wanariadha wanawake na wasichana kupitia , udhalilishaji na mathara ya upasuaji wenye madhara wa kimatibabu usio wa lazima kama njia ya kuruhusiwa kushiriki katika matukio mashindano ya michezo ya wanawake”.
Katika taarifa yao iliyochapishwa katika jarida la matibabu la Uingereza, hivi karibuni wataalamu walidai kuwa sheria za IAAF zinaitia katika hatari ya “kuweka viwango visivyo vya kisayansi kwa matukio mengine ya faida za maumbile “.
IAAF ilitaka kuweka sheria mpya tarehe 1 Novemba 2018, lakini ikakabiliwa upinzani wa kisheria uliolazimisha kusheleweshwa kwa utekelezwaji wake hadi Mahakama ya utatuzi wa migogoro ya michezo (Cas) itakapoamua juu ya suala hilo.
Wanariadha wa kike kama Caster Semenya wanatakiwa kukimbia na wanaume kulinga na sheria za IAAF
Chini ya sheria za IAAF, mwanariadha wa kike mwenye viwango asilia vya juu vya homoni za testosterone
Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa tarehe 26 Machi, lakini Cas iliiahirishahadi mwezi ujao.
Ushindi kwa Semenya utamfanya awe huru kuendelea kushiriki mashindano kama ambavyo amekuwa akifanya, lakini iwapo atashindwa kwenye kesi hiyo itamaanisha kuwa mwanariadha huyo wa Afrika Kusini anaweza kutoshiki mashindano, kushindana na wanaume au kulazimika kutumia dawa za kushusha viwango vyake vya homoni
Awali Semenya aliagizwa na wakuu wa riadha afanyiwe vipimo vya jinsia, lakini hakuna matokeo ya vipimo hivyo yaliyotangazwa rasmi kwa umma.
Testosterone ni homoni inayoongeza ukubwa wa misuli, nguvu za mwili na chembechembe nyekundu za damu,ambayo hathiri uwezo wa nguvu za mwili.
Katika taarifa iliyotolewa kwa BBC kitengo cha Spoti IAAF ilisema “ni wazi kwamba mwandishi wa ripoti hakuwahi kuona maelezo ya sheria za IAAF wala maelezo taliyowasilishwa hivi karibuni katika Mahakama ya utatuzi wa migogoro ya michezo.
” Kuna kauli ambazo si sahihi zilizomo kwenye muswada uliowasilishwa katika baraza la Haki za binadamu la umoja wa Mataifa kwa hiyo ni vigumu kujua ni wapi pa kuanzia.
” Tunalokubaliano sote ni kwamba tunaamini ni muhimu kuzingatia usawa katika mashinda ya michezo ya wanawake ili wanawake wawe huru kushiriki katika mashindano ya kitafa na kimataifa ya michezo .
” Kufanya hili ni muhimu ili kuhakikisha mashindano yaliyotengwa kwa ajili ya wanawake yanalindwa, jambo linalohitaji shertia na masharti ili kulilinda, vinginevyo tunajiweka katika hatari ya kupoteza kizazi kijacho cha wanariadha wanawake, kwani hawataona njia ya mafanikio katika michezo ya kike.”
RAY C ATOA SABABU KUTOMZIKA RUGE
UNJA ukimya! Sexy lady wa
Bongo Fleva, Rehema Yusuf Chalamila ‘Ray C’ ametaja sababu ya kutomzika
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
‘Jasiri Muongoza Njia’, Risasi Jumamosi lina habari kamili.
Kama ulikuwa hujui, mlezi mkuu wa Ray C kimuziki na kimaisha kwa
jumla alikuwa Ruge hivyo kifo chake hakiwezi kuwa ni jambo dogo kwa staa
huyo wa Wimbo wa Na Wewe Milele.
Ruge alifariki dunia Februari 26, mwaka huu nchini Afrika Kusini
alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo
kwa miezi kadhaa kisha kuzikwa kijijini kwao, Kiziru-Kabale, Bukoba
mkoani Kagera, Machi 4, mwaka huu.
RAY C HAKUONEKANA
Msiba wa Ruge uligusa na kuhudhuriwa na watu wengi wa kada mbalimbali wakiongozwa na Rais John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mawaziri na viongozi wengine huku wasanii wakiwa kama wote isipokuwa mwanadada Ray C. Wasanii wengi waliopitia mikononi mwa Ruge waliibua gumzo msibani, lakini Ray C hakuonekana.
MINONG’ONO MINGI
Kutoonekana kwa Ray C msibani kuanzia jijini Dar hadi kule Bukoba kuliibua minong’ono mingi kwa mashabiki wake wakitaka kujua kulikoni kwani wanajua Ruge alikuwa sawa na baba yake.
RAY C AELEZA SABABU
Katikati ya minong’ono na sintofahamu hiyo ya kutoonekana kwa Ray ndipo gazeti hili likajipa kazi ya kumtafuta mwanamuziki huyo almaarufu Kiuno Bila Mfupa ambaye alifunguka sababu ya kushindwa kufika kwenye msiba wa Ruge.
Katika mazungumzo yake na Gazeti la Risasi Jumamosi akiwa kwenye makazi yake jijini London, Uingereza, Ray C alisema wakati msiba huo unatokea alikuwa safarini kwenye ziara ndefu ya kimuziki nchini Marekani.
NI MSIBA MZITO
Ray C alisema kuwa, pamoja na kwamba ulikuwa ni msiba mzito kwake na kwamba alijikuta akitokwa machozi kutokana na uchungu wa kumpoteza mtu wake huyo wa karibu, lakini alishindwa kuahirisha au kuvunja ziara zake kwani alishalipwa kwa ajili ya shoo za watu. “Iliniuma sana, tena sana na mpaka sasa hivi inaniuma, natokwa na machozi kwa kumpoteza mtu muhimu kwangu.
“Nakumbuka wakati ninapata taarifa za msiba nilikuwa Marekani kwenye tour (ziara) kwa ajili ya shoo na nilishalipwa. “Kiukweli sikuwa na jinsi kwani nilishindwa kabisa kukatiza ziara,” alisema Ray C ambaye baada ya shoo za Marekani ataendelea na ziara yake nchini Ufaransa na Sweden.WARAKA WA RAY C KWA RUGE
Siku chache kabla ya kifo, Ray C alimwandikia Ruge waraka mzito akimtaka kuamka kitandani alikolazwa ili amwambie kinachoendelea maishani mwake. Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Ray C alimwandikia Ruge;
“Amka bwana, nimeshachoka kusubiri, meseji zangu hujibu, simu hupokei, nina stori kibao nataka kukwambia ingawa najua utanichamba, lakini nilishazoea kukwambia kila kitu changu kinachoendelea kwenye maisha yangu. “Tunagombanaga mpaka tunablokiana, lakini tukionana tu, tukaangaliana, tunabaki kucheka tu. “Nilishazoea kukwambia mambo yangu kwa sababu we’ ndo’ msiri wangu. We’ ndo’ unanipaga makavu nikiharibu.
“Kuna muda mpaka ninalia na ukiona ninalia, ndo’ unazidi kunipa makavu bila huruma. “Ninaondoka kwa hasira ingawa moyoni ninajua uliyoniambia ni kweli… ninakununiaaa ila haifiki wiki, huyo nimeshakuja ofisini kwako.
“Muda mwingine sina hata cha maana cha kukwambia ila nakuja tu ofisini kukuona unitanie nicheke! “Ray C umenimiss eeh… Kama nywele hujazielewa unanipa live Ray C nenda katoe hizo nywele.
“Nikikuona tu ninapata amani ya moyo. Nikitoka tu studio wa kwanza kukutumia demo! Ni wewe, wewe tu miaka yote tangu nimeanza muziki kwa sababu ninaheshimu sikio lako na ninaliamini.
“Mwezi wa ngapi sasa huu Ruge! Natuma meseji, ninakupigia, natamani kukuimbia japo kidogo upate nguvu sikupati…Ruge najua huko ulipo unaumia sana, najua unataka kuamka na kufanya kazi zako. Please wake up (tafadhali amka) babaa.
“Please! You are too strong (tafadhali wewe ni imara sana) babaa. Don’t give up please for you (usijikatie tamaa mwenyewe).
“Nishike mkono. Nibusu shavuni. Vyovyote vile. Nakupenda (wimbo unaoupenda sana). Amka Ruge.” Hata hivyo, pamoja na waraka huo mzito wa Ray C, lakini Ruge ambaye pia alikuwa meneja wa mwanadada huyo hakuamka hadi Mungu alipomchukua mja wake.
RAY C NI NANI?
Ray C aliyezaliwa Mei 15, 1982 mkoani Iringa ni mwimbaji wa R&B, Afro-Jazz na Taarab ambaye mkononi ana albamu nne za Mapenzi Yangu (2003), Na Wewe Milele (2004), Sogea Sogea (2006) na Touch Me (2008).
Ray C aliyesifika kwa kukata mauno alianza kujulikana baada ya kutoa nyimbo kadhaa kama vile, Sikuhitaji, Mapenzi Yangu, Na Wewe Milele, Ulinikataa na nyingine nyingi zilizompa umaarufu. Awali alikuwa mtangazaji wa Radio East Africa kabla ya kwenda Clouds FM na hatimaye kuwa mwimbaji maarufu aliyeutingisha na anayeendelea kufanya poa kwenye muziki wa Bongo Fleva.
MOBETO ACHARUKA, KISA DIAMOND
MWANAMITINDO Hamisa Mobeto juzikati alicharuka kinoma baada ya kuulizwa kuhusiana na madai ya mzazi mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’ kusitisha huduma za matunzo ya mwanaye Dylan. Awali, chanzo makini kililitonya Risasi Jumamosi kuwa, Mobeto kwa sasa anahaha baada ya kukosa matunzo kutoka kwa mzazi mwenzake huyo ambaye amesitisha mgao wa matunzo.“Mnajua Mobeto na Diamond kwa sasa ndiyo haziivi kabisa kwani amefikia hatua ya kushindwa kupewa matumizi ya mtoto, bi dada anahaha hajui la kufanya,” kilisema chanzo. Aidha, chanzo hicho kilidai kuwa, Mobeto kuna wakati anatamani hata angekuwa anapatana na mama wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ angeweza kumsaidia.
Hakuna maoni