Mwanafunzi akutwa ameuawa shambani
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Yungwe wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita, Alex Pastory amekutwa ameuwawa kwenye eneo la kichaka huku sababu za kifo hicho zikiwa bado azijajulikana.
Akizungumza
na Waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita, Mponjoli
Mwabulambo amesema marehemu wakati akiwa shuleni akiendelea na masono
aliomba ruhusa ya kwenda Nyumbani kwao ukerewe kwaajili ya matibabu
kutokana na hali ya afya yake kutokua nzuri.
Amesema,marehemu
alipewa ruhusa na kuondoka kwenda nyumbani na alivyo maliza matibabu
February 28 mwaka huu alirejea shuleni na kuendelea na masomo yake.
Aidha,Kamanda
Mponjoli amesema tangu Machi mosi mwezi huu mwanafunzi huyo alitoweka
shuleni pia hakuonekana katika maeneo ya nyumbani ambapo alikua
amepanga.
Sanjari
na hayo, Kamanda amesema ilipofika tarehe 8 mwezi huu mama mmoja ambaye
jina lake halikujulikana, wakati akiwa shambani analima aliona fuvu la
Binadamu kwenye eneo la shamba lake hali iliyomshitua na kupelekea
kuwaita wananchi na walipofika na kuchunguza walibaini kuwa ni mabaki ya
nguo za shule kuwepo kwenye eneo hilo.
Hakuna maoni