Coaster lililobeba wanafunzi lagonga treni na Kuua Mmoja.
Gari
la abiria lenye namba za usajili T930 DML aina ya Toyota Coaster
lililobeba wanafunzi wa sekondari limegonga Treni eneo la Kwamichi
Jijini Tanga na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi.
Basi
hilo lililokuwa limebeba wanafunzi wachezaji pamoja na washangiliaji
zaidi ya 30 liliweza kuburuzwa umbali wa mita 50 kutoka eneo ilipotokea
ajali .
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe akizungumzia ajali hiyo
iliyotokea jana Ijumaa Machi 15, 2019 amemtaja aliyefariki katika ajali
hiyo kuwa ni kondakta wa basi hilo ambaye jina lake halijatambulika mara
moja.
Majeruhi
waliofikishwa hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo ni wanafunzi 30
ambapo 19 kati yao hali zao si nzuri na madaktari wanaendelea na kuwapa
matibabu.
Hakuna maoni