Sarri: Wachezaji wa Chelsea wameshindwa kufikiria zaidi
Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri
alisema kuwa kushindwa kwao 2-0 na klabu ya Everton kuna maana ya
kwamba timu yake imefikia kikomo chake na hilo linaweza kuwa kweli
kutokana na sababu kadhaa
Raia huyo wa Itali alikuwa akielezea
kuhusu tofauti ya mchezo alioshuhudia katika kipindi cha kwanza na kile
cha pili ambapo alielezea kuwa mchezo mzuri zaidi alioshuhudia msimu
wote na kipindi cha pili ambapo alielezea kuwa timu yake ilikuwa
inacheza kana kwamba ilikuwa imefikia kikomo huku wachezaji wakiwa
wakishindwa kufikiria zaidi.Lakini pengine kikomo hicho kinaweza kutokana na ukufunzi wa kocha huyo , ikibainika kuwa haikuwa mara ya kwanza kwa kocha huyo mwenye umri wa iaka 60 kuishutumu timu yake msimu huu.
Na huenda ndio kikomo cha Chelsea kuwania nafasi nne bora hatua itakayomaanisha kwamba watalazimika kushinda kombe la Yuropa ili kufuzu kwa vilabu bingwa Ulaya.
Huku wakikabiliwa na mechi muhimu dhidi ya kikosi cha Marco Silva ambacho kilikuwa hakijashindwa na timu sita bora tangu mwezi Januari 2017, wageni hao walichanganyikiwa katika kipindi cha pili katika uwanja wa Goodison Park.
Chelsea ilipoteza kwa mara ya tano tangu mwaka huu uanze huku ikiwa ni Fulham pekee ilio na rekodi mbaya zaidi ukiwa ni mfano mwengine wa kikosi cha Chelsea ambacho kilishindwa kujibu kinapojipata nyuma kwa magoli.
Kushindwa kwao kunaiwacha klabu hiyo ya Sarri katika nafasi ya sita katika ligi ya Premia, pointi tatu nyuma ya Arsenal walio katika nafasi ya nne na kuzua maswali magumu ya iwapo Sarri ndio meneja atakayewaondoa katika matatizo yao kwa sasa.
Hakuna maoni