Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kuja Na Mkakati Wa Kuwa Na Mfumo Wa Kielektoniki Wa Kufuatilia Na Kuhifadhi Taarifa (Commodity Tracking System
Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma
Kutokana
na kukua kwa Technolojia kila siku, na matumizi ya techolojia
yanaongeza ufanisi, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza
na unaendelea na mkakati wa kuhakikisha kunakuwa na mfumo wa
kielektroniki wa kufuatilia na kuhifadhi taarifa za Hifadhi ya Taifa ya
Chakula (Commodity Tracking System).
Lengo
la kuwepo kwa mkakati huo ni kuongeza ufanisi kwa kupunguza mianya ya
udanyanyifu na wizi na ili kufikia lengo hilo ifikapo mwishini mwa mwaka
2020, Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umekubali kusaidia kupata
ufadhili wa fedha na utaalamu ili kufanikisha lengo hilo.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia Zikankuba wakati akizungumza kwa
niaba ya watumishi wenzake Kwenye hafla ya kukabidhi mtambo wa kusafisha
nafaka uliotolewa na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na kuzinduliwa na
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb).
Alisema
kuwa WFP ni mdau muhimu wa NFRA katika kuzungusha akiba ya chakula huku
Utekelezaji wa mauzo ya tani 36,000 ukiwa unaendelea.
Zikankuba
alisema kuwa mpaka sasa Tani zote zimekwisha andaliwa na WFP wamekwisha
kuchukua Tani 20,400 huku Tani 15,600 zikiwa zimekwisha andaliwa na
zimehifadhiwa vizuri kwa ajili ya WFP kuchukua.
“Mauzo
haya moja kwa maana yake ni kwamba Mkulima hasa mdogo anapata fursa ya
soko la kimataifa moja kwa moja kwa kuwa NFRA hununua mazao yake moja
kwa moja kutoka kwa wakulima” Alikaririwa
Bi
Zikankuba alitumia mkutano huo kuujulisha ujumbe wa WFP kuwa NFRA ipo
tayari na ina uwezo wa kuuza tani nyingine zaidi baada ya mkataba
unaoendelea wa Tani 36,000 kukamilika.
“Pia
tupo tayari kufanya mazungumzo na WFP ili kukusanya na kuwauzia mazao
mengine ya nafakai mtama kuanzia msimu ujao wa mavuno” Alisema
Aliongeza
kuwa Mikakati na programu mbalimbali zinazoendeshwa na WFP zinasaidia
NFRA kupata mazao yenye vigezo kupitia vikundi vya wakulima. Mfano:
Katika msimu huu, kati ya vikundi vya wakulima 216 vilivyouza mahindi
yao NFRA takribani vikundi 62 vilipata mafunzo ya kutunza na huhifadhi
mazao ya nafaka kupitia programu ya Farm to Market Alliance ya WFP.
Hakuna maoni