Tetesi za soka Ulaya Jumatano 24.04.2019: Felix, Zaha, Sane, Trippier, Gattuso, Mahrez, Hudson-Odoi, Coutinho, Richarlison

Mchezaji wa safu ya
kati wa Benfica Mreno Joao Felix ambaye sasa ana umri wa miaka 19 yuko
juu kwenye orodha ya uhamisho iliyotolewa na mshambuliaji wa Juventus
Cristiano Ronaldo, mwenye umri wa miaka 34, kwa klabu yake.
Washambuliaji wawili wa Ureno waliokuwa zamani katika Real Madrid -
Muhispania anayecheza safu ya kati Isco, 27, na mlinzi wa Ufaransa
Raphael Varane, mwenye umri wa miaka 25 - pia walikuwa kwenye orodha
hiyo. (Corriere dello Sport, via Mirror)

Crystal Palace watatakiwa kushusha bei yao ya £75m wanayotaka kumtoa Wilfried Zaha mwenye umri wa miaka 26 ikiwa mshambuliaji huyo wa Ivory Coast anataka kuhamia katika klabu ya Championi Ligi. Tottenham, Arsenal na Manchester United wogte wanamtaka lakini wanataka mkataba mzuri. (Star)
Manchester City wanahofu kuwa winga wao Mjerumani Leroy Sane, mwenye umri wa miaka 23, anaagalia uwezekano wa kuondoka kwenye klabu hiyo kutokana na kwamba mazungumzo ya mkataba wake yamekwama (Metro)

Kwa upande mwingine , United wanaamini Mbeljgiji Thomas Meunier mwenye umri wa miaka 27 anayechezea Paris St-Germain safu ya nyuma kulia ni mchezaji ambaye anayeweza kupatikana kwa bei nafuu na kwa urahisi zaidi anayeweza kukaba nafasi ya Trippier au Wan-Bissaka. (Independent)
- Jedwali la Msimamo wa ligi ya EPL 2018/19

Mshambuliaji wa Manchester City Riyad Mahrez anatishia kuondoka kwenye klabu hiyo na winga huyo Mualgeria mwqenye umri wa miaka 28, amekwisha lalamika wazi juu ya kunyimwa muda wa kucheza chini ya meneja Pep Guardiola. (Mail)
Hali ya baadae ya mchezaji wa safu ya kati wa Barcelona Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 26, itategemea ikiwa Fifa itaamua kuchelewesha marufuku ya kuhama dhidi ya Chelsea, huku Manchester United pia wakiwafuatilia kwa karibu wachezaji huyo maarufu wa Brazil . (Mirror)

AC Milan wanataka kusaini mkataba na mshambuliaji wa Everton Mbrazili Richarlison,mwenye umri wa miaka 21, hata hivyo klabu hiyo ya mabingwa wa Ligi ya Utaliano watatakiwa kuingia Championi Ligi na kulipa 75m euro kwa mujibu wa tathmini ya Ligi ya Primia. (Calciomercato)

Hata hivyo, meneja wa Arsenal Unai Emery anakabiliwa na kipindi kigumu cha kipindi cha uhamisho kutokana na hofu inayozingira klabu hiyo juu ya muswada wa malipo ya mshahara. (Mirror)

Stoke City wanadai £30m kwa ajili ya mlindalango Jack Butland mwenye umri wa miaka 26 kutoka Uingereza , anayelengwa na klabu za Primia Ligi Bournemouth na Crystal Palace. (Mail)
Ajax wako tayari kutoa mkataba mzuri wa muda mrefu kwa meneja Muholanzi Erik ten Hag mwenye umri wa miaka 49 ili kuzuwia klabu za Primia Ligi kumchukua. (Telegraph)
Norwich City watakuwa na ukomo wa bajeti ya £20m kwa ajili ya uhamisho kwani wanajiandaa kwa ajili ya Primia Ligi msimu ujao . (Mail)
Hakuna maoni