Header Ads

ad728
  • Breaking News

    Misikiti ni marufuku katika mji wa kale wa Aksum nchini Ethiopia

    Kwa wakristo wa kiorthodoksi nchini Ethiopia , mji wa kale wa Aksum ni mji tukufu, nyumbani kwa malkia wa Sheba aliyetajwa kwenye bibilia na sanduku la agano lililokuwa na amri 10 za Mungu.
    Inaarifiwa watawa katika mji huo wanakilinda sanduku hilo kilichokuwa na maamrisho hayo kumi aliyokabidhiwa Musa na Mungu.
    Makundi ya waislamu wanashinikiza kujenga msikiti katika mji huo - pendekezo linalopingwa na viongozi wa kikristo wanaosema wako radhi wafe kuliko hilo kufanyika.
    "Aksum ndio Mecca yetu," ametangaza kiongozi mkuu Godefa Merha, anayeamini kuwa kama makanisa yanavyopigwa marufuku katika mji mtukufu wa kiislamu, misikiti nayo hayaweza kuwepo katika mji wa kale wa Aksum.
    "Aksum ni eneo tukufu. Mji huu ni monasteri," anasema Godefa, naibu mkuu wa kanisa la Our Lady Mary of Zion mjini Aksum.
    Msimamo wa muda mrefu wa wakristu wa Orthodoksi sasa umegubikwa na mzozo wakati baadhiya waislamu wanashinikiza chini ya kauli mbiu "haki kwa waislamu wa Aksum" kuitisha haki ya kujenga msikiti katika mji huo na kuruhusu adhana ya kuwaita waumini kusali itangazwe kupitia vipaza sauti.
    Watu wengi wanaona mvutano huo ni wa bahati mbaya kwasababu ufalme wa Aksum, mojawapo wa ufalme wa jadi ulisifika kwa namna watu wa dini tofuati walivyokuwa wakiishi.
    Kwa mujibu wa waumini wa dini zote, waislamu waliwasili kwanza katika ufalme huo punde baada ya kuzuka kwa Uislamu mnamo 600 AD kama wahamiaji waliokwepa watawala wa Mecca wakati huo wasiokuwa waislamu.
    Mfalme wa kikriso aliwakaribisha na kuruhusu uislamu kuingia kwa mara ya kwanza katika eneo lililo nje ya rasi ya kiarabu.
    Hii leo, kuna takriban 10% ya waislamu katika idadi jumla ya watu wa Aksum jumla ya watu 73000 wanaoishi huko huku 85% yao wakiwa ni wakristo wa Orthodoksi na huku 5% wakiwa ni wa madhehebu mengine ya kikristo.
    'Waislamu walazimika kusali nje'
    Mkaazi wa kiislamu Abdu Mohammed Ali, aliye katika miaka ya 40, anasema kwa vizazi vingi familia yake imelazimika kukodi nyumba za wakristu kutoa nafasi kwa waisilamu kuabudu.
    "Kuna misikiti 13 ya muda. Siku ya Ijumaa iwapo [baadhi ya wakristo] wakitusikia tukitumia vipaza sauti, wanasema tunamdhalilisha St Mary," analalamika
    Aziz Mohammed, tabibu wa kitamaduni aliyeishi Aksum kwa miaka 20 anasema baadhi ya waislamu wanalazimika kusali nje hadharani kutokana na kukosekana misikiti.
    "Sisi waislamu hapa tunaishi na wakristo pamoja. Wakristu hawatuzuii kusali lakini kwa miaka mingi, wengi wetu tumekuwa tukisali katika maeneo ya wazi. Tunahitaji msikiti," anasema.
    Map
    Suala hilo ni wazi linazusha mzozo kati ya jamii. Abdu alikuwa na wasiwasi wa kuzungumza na mimi, mkristu wa Orthodoksi , na alifanya hivyo baada ya kumshawishi sana na baada ya kuangalia kitambulisho changu, huku Azizi ambaye alizaliwa na mama Mkristu na baba muislamu, akikataa kulizungumzia zaidi ya hapo suala hilo, na kusema: "Hapa tunaishi tukiogopana."

    Hakuna maoni

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728