Header Ads

ad728
  • Breaking News

    BONDIA AFALIKI DUNIA BAADA YA PAMBANO LAKE KUISHA.


    Bondia kutoka nchini Urusi, Maxim Dadashev amefariki dunia katika Hospitali ya UM Prince George, Maryland, United States baada ya pambano lake na Bondia, Subriel Matias katika pambano lao lililomalizika kwenye raundi ya 11 siku ya Ijumaa Julai 20, 2019.

    Imeelezwa kuwa Bondia huyo alipata majeraha katika kichwa chake, pamoja na kuvuja damu katika Ubongo wake.

    Dadashev amefariki akiwa na umri wa miaka 28 akiwa ameshinda mapambano 13 tangu aanze mchezo wa ngumi.https:


    Siku ya pambano lake hilo, Dadashev alishindwa kurudi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya Mkufunzi wake, Buddy McGirt kuona hali yakushangaza katika Afya yake.

    Shirikisho la Ngumi nchini Urushi limesema kuwa litafanya uchunguzi kuhusu Kifo cha Bondia huyo.

    Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo , Umar Kremlev amesema huenda kukawa na upuuzwaji, ameongeza kuwa tumempoteza Maxim Dadashev. Ni kijana yetu mdogo sana, "Tupo tayari kumsaidia pamoja familia yake ikiwa na masuala ya kifedha"

    Hakuna maoni

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728