Header Ads

ad728
  • Breaking News

    Rais wa Tanzania John Magufuli apokea dhahabu na fedha zilizokamatwa Kenya



    Serikali ya Tanzania imepokea kilo 35.34 za madini ya dhahabu zenye thamani ya dola milioni moja za Marekani na fedha kiasi cha shilingi milioni 170 za Tanzania, dola za Marekani 76,500 na shilingi za Kenya 171,600, fedha zilizokamatwa nchini Kenya.
    Mali hiyo ilikamatwa tangu mwaka 2004 baada ya kuibwa kwenye benki ya NBC tawi la Moshi.
    Ujumbe wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ukiongozwa na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Monica Juma na Mkurugenzi wa mashtaka Nurdini Haji, umekabidhi madini na fedha hizo Ikulu ya Tanzania na kutoa ripoti kuhusu namna madini hayo yalivyokamatwa mwaka jana nchini Kenya.
    Mkurugenzi wa mashtaka wa Tanzania, Biswalo Mganga, aliongoza timu ya watu 11 kuhakikisha dhahabu iliyokamatwa inarejea ili kuweza kutumika kama kidhibiti kwenye kesi inayoendelea kuhusu makosa ya uhujumu uchumi huko Mwanza.
    Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Monica Juma
    Waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Monica Juma

    Dhahabu zilipatikanaje?

    ''Mnamo tarehe 15.2.2018 dhahabu ya kilo 35.34 wakati msafiri mmoja ajulikanaye kwa jina la Baraka Chaulo aliyesafiri na ndege ya shirika la Presicion akitokea jijini Mwanza, kisha kutua Kilimanjaro na baadae kuelekea Kenya alipokamatwa kwenye uwanja wa Jommo Kenyatta..taarifa zilipopatikana, mkurugenzi wa upelelezi wa Tanzania na mwenzake wa Kenya walishirikiana kufanyia upelelezi tukio hilo''.
    Mganga amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Profesa Adelardus Kilangi aliandika maombi kwenda Kenya kuomba dhahabu hiyo irejeshwe.
    Amesema pia taratibu za kumrejesha nchini kutoka Kenya mtu aliyeshiriki uvamizi katika benki ya NBC tawi la Moshi zilikwama kwa miaka mingi, lakini kwa ushirikiano kati yake na DPP wa Kenya, mshtakiwa huyo ameshejeshwa Tanzania na kesi yake iko Moshi.
    "Namshukuru Rais Kenyatta kwa upendo na uaminifu mkubwa alionao kwa kurejesha dhahabu yenye uzito wa kilo 35 pamoja na fedha, rais Uhuru amefanya kitendo cha kiungwana kwa kuturudishia madini yetu ambayo yalikuwa yametoroshwa.
    "Navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa kazi kubwa walioifanya."Tuliamua kuchukua hatua za makusudi za kuweka mikakati ya kulinda rasilimali zetu za madini ili ziweze kuwanufaisha Watanzania''.
    Kwa mujibu wa rais Magufuli matukio ya utoroshaji wa madini nchini Tanzania yamefika 102 kwa mwaka uliopita pekee.
    "Wa kupongezwa kwa hili ni vyombo vya Kenya, najua wakuu wa vyombo hivyo Tanzania mpo hapa, lazima niwatandike kwa sababu vitu vimetoka Mwanza vimekamatiwa Kenya. Je, vilipobebwa Mwanza na Kilimanjaro vyombo vyetu vilikuwa vinafanya nini?
    'Vitu vya fedha na dhahabu vinahitaji moyo wa jiwe, kiukweli Rais Kenyatta ni muaminifu, kwani vingeweza kupigwa, lakini fedha hizi zimerudi Tanzania baada ya miaka 15. Lakini na mimi mnipongeze, inawezekana wengine wangepiga dili juu kwa juu na wala msingejua.

    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akipokea kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma Dhahabu pamoja na pesa iliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019

    Hakuna maoni

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728