Header Ads

ad728
  • Breaking News

    Ndege mpya aina ya Boeing 737 yaanguka baada ya kupaa Jakarta, Indonesia

    Jamaa za abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo wameanza kufika kituo cha huduma za dharura uwanja wa ndege wa Jakarta wa Soekarno Hatta October 29, 2018.
    Ndege ya kuwabeba abiria ya shirika la Lion Air aina ya Boeing 737 imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege mjini Jakarta, maafisa wa Indonesia wamesema.

    Ndege hiyo safari nambari JT-610 iliyokuwa imewabeba abiria 188 ilikuwa safarini kutoka mji huo mkuu wa Indonesia kwenda Pangkal Pinang, jiji linalopatikana katika visiwa vya Bangka Belitung.
    Iitoweka kutoka kwenye mitambo ya rada saa kadha baada ya kupaa, ilipokuwa inavuka bahari.
    Katika kikao na wanahabari, maafisa wamesema ndege hiyo, ambayo ni ndege mpya aina ya Boeing 737 MAX 8, ilikuwa imewabeba abiria 178 watu wazima, watoto watatu, marubani wawili na wahudumu watano wa ndege.
    Yusuf Latif, msemaji wa shirika la huduma za uokoaji na kuwatafuta manusura amewaambia wanahabari: "Imethibitishwa kwamba ndege hiyo imeanguka."
    Maafisa wa uokoaji wakiwa eneo ambalo ndege hiyo ilianguka

    Hakuna maoni

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728